Tuesday, March 24, 2020

Tahadhari Covid-19 mjini Moshi zaendelea kuchukuliwa

Kituo cha Mabasi cha Moshi-Holili kilichopo mjini Moshi ni miongoni mwa maeneo ya mfano katika mapambano dhidi ya maambukizo ya virusi vya Corona ambapo utaratibu wa kunawa kabla hujaingia katika basi kuendelea na safari ni lazima unawe mikono.

Utekelezaji wake ulianza Machi 23, 2020 pale abiria walipotakiwa kunawa mikono kabla ya kuingia katika basi huku chombo cha kunawia mikono kikiwa karibu na mlango wa kuingia katika basi.

Dereva aliyetambulisha kwa jina Kassim alisema wamekubaliana na uongozi wa Muungano wa Madereva wa Moshi-Holili kuhamasisha ili kukabiliana na maambukizi ya Covid-19 na abiria ambaye hataki kunawa haruhusiwi kuingia katika basi.

Aidha tahadhari hiyo imepokelewa pia maeneo mengine wilayani humo, kama migahawa na katika maeneo ya kazi binafsi na umma.





0 Comments:

Post a Comment