Tuesday, March 10, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Harriet Tubman ni nani?

Machi 10, 1913 alifariki dunia mkomeshaji wa biashara ya utumwa nchini Marekani Harriet Tubman. Mwanaharakati huyo alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.

Wakati akiwa utumwani alikuwa akipigwa makofi, kuchapwa na mabwana (wakuu) tofauti. Alipokuwa mdogo sana, mwangalizi mwenye hasira alishika chuma chenye uzito mkubwa akiwa na malengo ya kumjeruhi mtu mwingine, kwa bahati mbaya chuma hicho kilimpiga Tubman kichwani. 

Hiyo ilisababisha narcoleptic, maumivu ya kichwa, maono yenye nguvu na alianza kujiwa na ndoto kutokana na majeraha hayo. Alikuwa na matatizo hayo maisha yake yote. Tubman aliamini kuwa maono na ndoto wazi hutoka kwa Mungu.

Biashara ya watumwa ilikuwa biashara iliyodhalilisha utu wa binadamu, hasa Waafrika ambao ndio waliotumika kwa kiasi kikubwa katika biashara hiyo. 

Baadhi ya watu Ulaya waliweza kuona madhara mbalimbali yaliyotokana na biashara hiyo hatarishi, na kuamua kuanzisha tapo la kuikomesha. Wengi wao walikuwa watu wa dini waliosukumwa na sababu za ubinadamu.

Baadaye mataifa kama Uingereza yaliongeza bidii katika ukomeshaji wa biashara ya utumwa. Kwa kiasi fulani ukomeshaji wa biashara ya utumwa ulikuwa una manufaa ya kiuchumi kwao, hasa kufuatia matokeo ya mapinduzi ya viwanda yaliyotokea nchini mwao.

Hata hivyo msukumo mkubwa wa Harriet Tubman ambaye mwaka wa 1849 alitoroka kwenda Philadelphia. Huko watumwa walikuwa huru. Baadaye alirudi Maryland ili kuwaokoa familia yake. Hatimaye aliongozwa na watumwa wengine wa uhuru. 

Wamiliki wa watumwa walitoa zawadi kubwa kwa kurudi kwa watumwa wao. Tubman hakuwahi kushikwa kwa sababu hakuna mtu aliyefahamu kwamba alikuwa akiwaacha huru watumwa.

Wakati anatoroka mwaka 1849 Tubman alianza kuugua bwana wake Edward Brodess alikuwa akijaribu kutaka kumuuza lakini hakuweza kupata mnunuzi. Tubman alimkasirikia bosi wake kwa kutaka kumuuza na pili kwa kuendelea kuwashikilia utumwa ndugu zake. 

Tubman aliwahi kusema alianza kuomba kwa Mungu kuhusu bosi wake, akimtaka Mungu afanye mabadiliko katika njia zake.  

Baadaye akaendelea zaidi kumtafuta Mungu, " I prayed all night long for my master till the first of March; and all the time he was bringing people to look at me, and trying to sell me."  ikiwa na maana kwamba muda wote alikuwa akiomba Mungu lakini cha kustaajabisha Brodess aliendelea kuwaleta watu kwa ajili ya kumwangalia ili waweze kumnunua.

Hata hivyo Tubman alipoona hakuna mabadiliko alimwambia Mungu, "I changed my prayer. First of March I began to pray, 'Oh Lord, if you ain't never going to change that man's heart, kill him, Lord, and take him out of the way." Ikiwa na maana kwamba kama Mungu hawezi kumbadilisha Brodess moyo wake katika hilo basi amwue, amwondoe katika ulimwengu huu. 

Na Mungu akawa mwaminifu kwa maombi ya Tubman juma moja baadaye Brodess alifariki dunia.

Tubman alizaliwa akipewa jina la Araminta 'Minty' na wazazi wake Harriet 'Rit' Green na Ben Ross.  

Rit alikuwa mikono mwa Mary Pattison Brodess. Ben aliuzwa kwa Anthony Thompson. 

Mary Brodess alikuja kuwa mume wake wa pili. Wawili hao walikuwa na mashamba makubwa karibu na mto Blackwater huko Madison katika kaunti ya Dorchester, Maryland. 

Hivyo kumiliki watumwa wengi ilikuwa ni kitu cha kawaida. Miongoni mwa hao ndio wazazi wake Harrieth Tubman. Tubman alizaliwa huko huko Maryland huku wanahistoria wakishindwa kujua ni mahali gani lakini wote wanakubaliana kwamba mwanaharakati huyo alizaliwa utumwani. 

Mtunzaji wa rekodi Kate Larson aliweka kumbukumbu kwamba Tubman alizaliwa mwaka 1822 wakati huo huo Jean Humez alisema Tubman alizaliwa mwaka 1820. Catherin Clinton aliweka kumbukumbu kwamba Tubman alizaliwa mwaka 1825. 

Hata hivyo cheti chake cha kifo kinataja kuwa alizaliwa mwaka 1815 huku kaburi lake likiandikwa mwaka 1820. Inaelezwa kwa bibi yake upande wa mama yake alitua katika ardhi ya Marekani kwa meli ya watu kutoka barani Afrika. 

Hakuna taarifa zaidi kuhusu ndugu wengine. Akiwa mtoto Tubman alikuwa akiambiwa kuwa asili yake ni watu wa Ashanti ambayo kwa sasa ni Ghana. 

Na hiyo ilitokana na mwonekano wake na tabia zake. Mama yake alikuwa mpishi katika familia ya Brodess. 

Baba yake alikuwa mahiri katika uchongaji wa vifaa vya miti ambaye alipewa majukumu ya kusimamia shamba la Thompson. 

Walioana miaka ya 1808 ana kwa mujibu wa rekodi  za mahakamani walikuwa na watoto wa tisa walioishi nao ambao ni Linah, Mariah Ritty, Soph, Robert, Minty (Harriet), Ben, Rachel, Henry, and Moses

Wakati Vita nchini Marekani inaanza, Tubman alifanya kazi katika Jeshi la Muungano. 

Alifanya kazi kwanza kama mpishi na muuguzi. Baadaye alikuwa shujaa wa silaha (scout) na mpelelezi. Alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza kundi la silaha (scout) katika vita. Aliongoza uvamizi wa Mto Combehee, ambao uliwaokoa watumwa zaidi ya 700 huko South Carolina.

Baada ya vita, alirudi nyumbani kwake Auburn, New York kuwalea wazazi wake. Alianza kufanya kazi kama mwanaharakati (mwanamke mwenye shauku) huko New York hadi alipoanza kuwa mgonjwa.

Karibu na mwisho wa maisha yake, aliishi nyumbani kwa mababu zake wa Afrika. Miaka kadhaa kabla, alisaidia kurekebisha nyumba hiyo.

0 Comments:

Post a Comment