Machi 14, 1883 alifariki dunia mwanafalsafa wa Ujerumani Karl Marx.
Mwanafalsafa huyo na mwenzake anliyefahamika kwa jina la Friedrich Engels ndiye mwanzilishi wa Ukomunisti.
Baada ya kifo cha mkewe aliyefahamika kwa jina la Jenny mnamo Desemba 1881, Marx alianza kudhoofu kutokana na viriba hewa kuvimba na kujawa na utando ambao ulisababisha kifo chake.
Homa hiyo ilimkamata kwa miezi 15 ya mwisho ya maisha yake.
Machi 14, 1883 akiwa jijini London alipoteza maisha akiwa na umri wa miaka 64.
Familia na marafiki zake walimzika London kwasababu hakuwa na uraia wowote wakati huo kutokana na sheria zilizokuwepo.
Alizikwa katika makaburi ya Highgate Mashariki mwa London mnamo Machi 17, 1883 pembeni ya kaburi la George Eliot.
Eneo hilo la makaburi liliwekwa kwa ajili ya watu ambao haawamini uwepo wa Mungu. Katika mazishi hayo kulikuwapo watu wasiozidi 11.
Hata hivyo kuhusu hali yake ya afya Mwandishi wa biografia yake Werner Blumenberg aligusia kuwa na tatizo la ini na nyongo kwamba Marx alianza kupatwa na changamoto hiyo tangu mwaka 1849 na haikuwahi kumweka huru hadi mauti yake kutokana na aina ya maisha aliyokuwa akiishi.
Blumenberg aliandika kuwa mashambulio hayo mara nyingi yalimwandamana Marx kwani kuna wakati alipatwa na maumivu ya kichwa, kuvimba jicho, nyurolojia ya kichwa na maumivu ya koo ambayo yalitokana na rumatizimu.
Rumatizimu ni ugonjwa wa kuvimba unaoweza kuhusisha moyo, jointi, ngozi, na ubongo. Ugonjwa huu hujijenga majuma mawili hadi manne baada ya maambukizi ya koo.
Mnamo mwaka 1877 ndipo ilijidhihirisha wazi kuwa Marx alikuwa na matatizo hayo. Blumenberg aliongeza kwamba kudhoofu kiafya kulikuja kwa mwanafalasafa huyo kutokana na kazi nyingi za usiku na lishe mbovu.
Mbali na kuwa mwanafalsafa alikuwa mchumi, mwanahistoria, mwanamapinduzi wa Kishoshalisti, mwananadharia wa kisiasa na kijamii, mwandishi wa habari na mwanasiasa.
Marx alisoma sheria na falsafa katika chuo kikuu. Aliolewa na Jenny von Westphalen mnamo 1843.
Kwa sababu ya machapisho yake ya kisiasa, Marx hakuwa na jina na aliishi uhamishoni na mkewe na watoto huko London kwa miongo kadhaa, ambapo aliendelea kukuza wazo lake kwa kushirikiana na mfikiriaji wa Ujerumani Friedrich Engels na kuchapisha maandishi yake, kutafiti katika chumba cha kusoma cha Makumbusho ya Uingereza.
Majina yake maarufu zaidi ni kijitabu cha 1848, Manifesto ya Kikomunisti, na Das Kapital (Toleo la Tatu). Marx amekuwa mtu wa kukumbukwa hadi sasa.
Mawazo yake ya kisiasa na kifalsafa yalikuwa na ushawishi mkubwa juu ya historia ya baadaye ya kiakili, kiuchumi na kisiasa, na jina lake limetumika kama kivumishi, nomino na shule ya nadharia ya kijamii.
Kwa Marx kazi ya falsafa haikuwa kueleza dunia ilivyo bali kuibadilisha.
Alifundisha ya kwamba mawazo, fikra na imani zote zinatokana na hali ya uchumi na teknolojia katika jamii.
Mwenyewe aliathiriwa sana na Georg Wilhelm Friedrich Hegel na kutoka kwake alipokea hoja ya kuwa historia inafuata kanuni zake likielekezwa kwenye lengo maalumu.
Tofauti na Hegel, Marx aliona historia haisukumwi na "roho ya ulimwengu" bali na nguvu za uchumi wa jamii na namna ya kujipatia riziki za maisha.
Kutokana na msingi huu Marx alikataa dini na imani ya Mungu.
Kwake dini ni itikadi ya jamii ya uwongo na pamoja na sahihisho la jamii alitarajia ya kwamba dini itapotea.
Marx aliathiri pakubwa kubwa kati ya vyama vya wafanyakazi vya Ulaya vyenye mwelekeo wa kisoshalisti. Baadaye kundi kali kati ya wasoshalisti Warusi chini ya Lenin iliendelea kupanua mafundisho ya Marx kwa "Umarx-Ulenin" iliyokuwa itikadi rasmi ya vyama vya kikomunisti.
Marx aliheshimiwa kama nabii katika nchi zilizotawaliwa na Wakomunisti, kuanzia Urusi hadi kuenea kwa thuluti moja ya watu wote duniani.
Mwishoni mwa miaka ya 1980 heshima yake ilipungua kutokana na anguko la Urusi.
Marx alichapisha kazi nyingi ikiwamo ya "The Poverty of Philosophy" ambapo mwaka 2017 ilikuwa ikitimiza miaka 170 tangu kuchapishwa kwa kazi hiyo mwaka 1847. Marx aliandika ikiwa ni kumjibu mwandishi Pierre-Joseph Proudhon's System of Economic Contradictions ambaye aliandika mwaka mmoja kabla ya Marx.
Baada kifo chake Engels aliendelea kuchapisha kazi alizofanya na Marx, katika Manifesto ya Ukomunisti, inaanza kwa kuandikwa "Ninasikitika kusema kuwa utangulizi wa mchapo huo wa sasa lazima niutie sahihi реке yangu.
Marx, mtu ambaye tabaka nzima ya wafanya kazi katika Ulaya na Marekani inamfuata yeye kuliko mtu yeyote mwingine, hivi sasa amelala katika kiunga cha Highgate na juu ya kaburi lake majani yameshaanza kuota. Tangu kufa kwake, ndio zaidi hapatakuwa na fikira ya kuyabadilisha au kuyaongeza "Maelezo" hayo. Ndio. Zaidi ninahisi kuwa kuna uhitaji wa kuyaelezea hapa." Hayo yalisemwa na Engels Juni 28, 1883 ikiwa ni miezi mitatu baada ya kifo cha Marx.
Januari 30, 1888 Engels akiwa jijini London alisema, "Maelezo” haya yakiwa ni kazi yetu ya pamoja, ninajihisi imenipasa nielezee kwamba fikira muhimu, ambayo ndiyo kiini cha "Maelezo” hayo, inatokana na Marx."
Mapinduzi ni mabadiliko ya haraka upande wa siasa na miundo yanayotokana na shinikizo la wananchi, linalotumia mara nyingi nguvu.
Katika historia ya binadamu mapinduzi yalitokea mara nyingi kwa sababu, mbinu, muda na malengo mbalimbali. Hayo yalifuatwa na athari kubwa juu ya utamaduni na uchumi wa jamii husika.
Februari 1, 1893 Engels katika maandiko yake kuhusu Marx katika Ilani ya Ukomunisti au Manifesto ya Ukomunisti alisema Uchapaji wa Maelezo ya Chama cha Kikomunist umetokea kwa bahati, mtu anaweza kusema, karibu na tarehe 18 Machi mwaka 1848, siku уa Thawra au siku ya mapinduzi ya Milan na Berlin ambayo yalikuwa ni mapigano ya silaha ya nchi mbili hizo zilizokuwa katikati, moja katika bara la Ulaya na ya pili katika nchi za Mediterranean; nchi mbili ambazo mpaka wakati huo zilidhoofishwa kwa migawiko na matatizo ya ndani, na kwa hivyo zikaangukia chini уa utawala wa kigeni.
Wakati huo Italia ilikuwa mikononi mwa mfalme wa Austria, na Ujerumani ilikuwa katika utumwa wa mfalme wa Urusi,
Engels aliongeza kuwa kama ilivyokuwa, kwa Karl Marx kila mahali mapinduzi (thawra) imekuwa ni kazi ya tabaka la wafanyakazi; kwani wao ndio waliojenga maboma na kuyatoa maisha yao.
0 Comments:
Post a Comment