KWA UFUPI KUHUSU JIMMY SHOJI
Jimmy Shoji ni miongoni mwa wachezaji waliopo katika kikosi cha Polisi Tanzania katika nafasi ya kiungo.
Jina lake halisi ni Jimmy Shoji Mwaisondola. Akiwa na Polisi Tanzania amekuwa akivaa jezi Na. 20; hivyo unapoona namba 20 dimbani basi ujue ni Jimmy Shoji.
Amekuwa mcheza muhimu katika kikosi hicho akiwa amesheheni uzoefu mkubwa na maarifa ya soka katika nafasi hiyo.
Shoji sio mgeni na soka la Tanzania kwani ujio wake haukuja mara moja alianza kuhudumu na timu mbalimbali hapa nchini Tanzania Mbeya Mashujaa, Njombe Mji na Lipuli.
Ujio wa kocha Selemani Matola katika kikosi cha Polisi Tanzania akitokea Lipuli ya Iringa ulimleta nyota huyo ambaye amekuwa muhimu katika safu ya kiungo ya Polisi Tanzania.
Amecheza kwa kujituma na kuchangia mafanikio katika msimu wa kwanza wa Polisi Tanzania Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020.
Anapokuwa na mafundi wengine kama Hassan Maulid Machezo, Baraka Majogoro, Pato Ngonyani na Marcel Kaheza hakika eneo hilo lazima viungo wa timu pinzani wawe kwenye wakati mgumu wa kuwanyang'anya mipira.
Miongoni mwa michezo aliyocheza ni ule wa Machi 14, 2020 dhidi ya Ndanda FC uliomalizika kwa ushindi wa bao 1-0.
Mtanange huo ulichezwa katika Uwanja wa Ushirika, Moshi kukishuhudiwa kiungo huyo akishindwa kumaliza baada ya kupata majeruhi.
Kabla ya kutoka Shoji alifanya kazi nzuri ambayo ingezaa matunda basi baaab kubwa.
Kazi hiyo ilikuwa kumimina krosi iliyomkuta Iddy Mobby aliyeikandamiza kwa kichwa na kuishia kugonga mhimili wa goli upande wa chini kaskazini.
Shoji alipata majeraha ambayo yalimlazimisha Kocha Malale Hamsini kumtoa na kumwingiza Andrew Chamungu.
Kikosi cha Polisi Tanzania kiliundwa na; Peter Manyika Jr. Shaban Stambuli, Juma Haji. Iddy Mobby, Mohamed Kassim, Baraka Majogoro, Jimmy Shoji, Hassan Maulid, Mohamed Mkopi, Marcel Kaheza na Mateo Anthony.
Wa Akiba; Mohamed Ali, Pato Ngonyani, Andrew Chamungu, Mohamed Mmanga, Pius Buswita, Henrico Kayombo na Krote Samson.
STORY & PHOTO BY: Jabir Johnson
EMAIL: jabirjohnson2020@gmail.com
DATE: Machi 14, 2020
0 Comments:
Post a Comment