Machi 9, 2005 nyota wa soka Clint Dempsey alianza vema majukumu yake ya kuitumikia timu ya taifa ya Marekani kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Colombia.
Kiungo mshambuliaji huyo alianza kuhudumu Novemba 2004 na miamba hiyo ya Amerika ya Kaskazini lakini hakuwahi kuanza katika kikosi cha kwanza.
Mchezo wa kirafiki dhidi ya Colombia ulitoa mwanya kwa Dempsey kuonyesha makeke yake na matarajio kwa siku za usoni.
Kinachovutia zaidi alianza katika kikosi cha kwanza katika siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake akifikisha miaka 22.
Dempsey alikuwa miongoni mwa wachezaji sita waliokuwa wakianza kwa mara ya kwanza kuhudumu na timu ya taifa akiwamo mlinda mlango Jon Busch na Chad Marshall.
Pia katika mchezo huo kulikuwa na wachezaji wawili waliokuwa wanafanana majina ya kwanza na Dempsey alikuwa miongoni mwa hao Clint wawili.
Bao la dakika 25 lilifungwa na nyota kutoka New England Revolution Pat Noonan akipokea pasi ya mwisho kutoka kwa nyota wa mwenzake kutoka klabu moja Steve Ralston. Ralston alitoa pasi ya mwisho katika bao la pili lililofungwa na Marshall katika dakika ya 33.
Na Clint Mathis alifunga ala tatu katika dakikaa ya 66 ya mchezo dhidi ya Colombia.
Licha ya kwamba Dempsey hakufunga bao katika mchezo huo lakini aliweka rekodi ya kufumania nyavu mara 57 katika mechi 141 na kumfanya kuwa mfungaji bora wa zama zote wa Marekani katika timu ya taifa hilo.
0 Comments:
Post a Comment