Machi 10, 1925 ilianzishwa klabu ya soka ya Olympiacos baada ya mgawanyiko uliojitokeza.
Kuanzia hapo Olympiacos imekuwa ni klabu yenye mafanikio makubwa nchini humo ikitwaa mataji 44 ya ligi kuu, Vikombe vya Ligi 27 kati ya hivyo 17 ilichukua mara mbili mfululizo na Mataji manne ya Super Cup.
Kwa ujumla Olympiacos ina mataji 75 hivyo kuwa timu ya soka yenye mafanikio makubwa nchini Ugiriki. Olympiacos inashika nafasi ya 9 kwa kutwaa mataji mengi duniani.
Klabu nyingine nchini Ugiriki zimechukua mataji 39 ya Ligi. Pia Olympiacos iliweka rekodi ya kutwaa mataji ya ligi kuu nchini humo mara saba mfululizo mnamo mwaka 1997 hadi 2003 na ikafanya hivyo tena mwaka 2011 hadi 2017.
Rekodi hiyo ilivunja ile ya mara sita iliyowekwa miaka ya 1950.
Olympiacos hufahamika kwa jina jingine kama Thrylos (Greek: Θρύλος) ikiwa na maana ya Mkongwe.
Miamba hiyo imekuwa ikipata uungwaji mkono kote duniani na pia imekuwa klabu maarufu sana katika jiji la Athens.
Mpaka April 2006 ilikuwa imewasajili wanachama akali ya 83,000. Pia mwaka huo huo ilishika nafasi ya tisa kwa kuwa klabu ya soka yenye wanachama wanaolipa vizuri.
Namba hiyo iliongezeka mwaka 2014 na kufikia wanachama 98,000.
Tangu kuanzishwa kwake uhasama uliibuka baina yao na Panathinaikos hivyo uhasama huo unafahamika kama " Uhasama wa Maadui wa Mbinguni" Huu ndio utani wa jadi wa muda mrefu nchini Ugiriki na unafahamika duniani kote.
Mpaka sasa Olympiacos inaongoza kwa kuizabua mara nyingi zaidi Panathinaikos ikishinda mara 82 na kushindilia mabao 265. Januari 5, 2020 Olympiacos ilishinda kwa bao 1-0.
Rangi za klabu hiyo ni nyekundu na nyeupe. Na Olympiacos ilikuwa timu za mwanzoni kabisa kuanza kucheza ligi kuu nchini Ugiki msimu wa 1927-28.
Taji la kwanza ililipata mwaka 1931 na baada ya hapo Olympiacos ilichukua mara tano katika misimu saba.
0 Comments:
Post a Comment