Thursday, March 5, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Hugo Chavez ni nani?

Machi 5, 2013 alifariki dunia mwanasiasa wa Venezuela na Rais wa 45 wa taifa hilo Hugo Chavez. 

Mwanasiasa huyo tishio la ubeberu wa Magharibi alihudumu kama kiongozi wa taifa hilo kutoka mwaka 1999 hadi kifo chake mwaka 2013. 

Makamu wa Rais Nicolas Maduro alitangaza katika televisheni ya taifa kuwa Chavez amefariki dunia katika hospitali ya kijeshi jijini Caracas majira ya 10:25 jioni kwa saa za Venezuela nchini Tanzania ilikuwa ni saa 10:25 asubuhi. 

Maduro alisema Chavez amefariki dunia baada ya kuupigania uhai wake kwa takribani miaka miwili. Kutokana na taarifa za watu wa karibu zilionyesha kuwa Chavez alifariki dunia  kutokana na shambulio la moyo na saratani ya utumbo mkubwa. 

Jenerali Jose Ornella ambaye alikuwa karibu sana Chavez katika dakika zake mwisho alisema hakuwa na uwezo wa kuzungumza kwa sauti lakini maneno yake ya mwisho yalikuwa:  "Yo no quiero morir, por favor no me dejen morir" ikiwa na maana ya " Sipendi kabisa kufa. Tafadhali usiniache nife. Chavez aliacha watoto wanne na wajukuu wanne  

Mnamo Juni 2011 iliripotiwa na televisheni za Cuba kuwa Chavez alikuwa akipata nafuu baada ya upasuaji wa kuondoa uvimbe katika seli zake. 

Makamu wa Rais wakati huo Elias Jaua aliweka bayana kuwa Chavez anaendelea vizuri hivyo hakukuwa na haja ya kukaimisha madaraka licha ya kutokuwepo kwake nchini Venezuela. 

Julai 17, 2011 taarifa za habari katika televesheni ziliripoti kuwa Chavez amerudi nchini Cuba kwa ajili ya kupata matibabu zaidi ya saratani. Chavez alionekana hadharani Julai 28, 2011 wakati wa Kumbukizi ya kuzaliwa kwake wakati huo alikuwa akifikisha miaka 57 ambapo katika hotuba yake alizungumzia hali yake ya afya. 

Baada ya hotuba yake mwezi mmoja baadaye Chavez alitangaza kuwa serikali yake itachukua migodi ya dhahabu iliyokuwa mikononi mwa Russia kupitia kampuni ya Rusoro. Pia Chavez alitangaza kuondoa stock za dhahabu  zilizokuwa katika benki za magharibi na kuwapa washirika wake wa kisiasa Russia, China na Brazil.

Chavez alizaliwa Julai 28, 1954. Alikuwa kiongozi wa Fifth Republic Movement kutoka kuanzishwa kwake mwaka 1997 mpaka 2007 kilipoungana na vyama vingine kuunda United Socialist Party of Venezuela (PSUV), na aliongoza chama hicho mpaka 2012.

Alizaliwa katika familia ya watu wa kawaida waliotegemea kipato kwa kufanya kazi katika mji wa Sabaneta, Barinas, Chavez alikuja kuwa ofisa wa jeshi na hakuridhika jinsi wanasiasa wa Venezuela walivyojikita kwenye Punto Fijo Pact, alianzisha kwa siri Revolutionary Bolivarian Movement-200(MBR-200) mwanzoni mwa miaka ya 1980. Chavez aliongoza MBR-200 katika mpango wa kupindua serikali ya Democratic Action iliyoongozwa na Rais Carlos Andres Perez mnamo 1992, na kwasababu hiyo alifungwa jela.

Alipotoka jela baada ya miaka miwili, alianzisha chama cha siasa kilichojulikana kama Fifth Republic Movement na alichaguliwa kuwa rais wa Venezuela mwaka 1998. Alichaguliwa tena mwaka 2000 na tena mwaka 2006 kwa jumla ya asilimia 60 ya kura zote.

Baada ya kushinda muhula wa nne wa urais katika uchaguzi wa mwezi Oktoba 2012 ilikuwa aapishwe January 10 2013, lakini Bunge liliahirisha sherehe hizo za kuapishwa ili kumpa nafasi ya afya yake kuimarika kutoka kwani alikuwa anatoka kwenye matibabu nchini Cuba. 

Alisumbuliwa na saratani iliyogundulika Juni 2011, Chavez alikufa alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 58.

Kufuatia mpangilio wa mfumo 1999, Chaves alilenga katika kuamuru mabadiliko katika huduma za jamii katika Bolivarian Revolution, hii ilikuwa kama sera ya ujamaa. 

Kutumia tarakimu za mapato ya mafuta miaka ya 2000 serikali yake ilipitisha ushirikiano wa kidemokrasia uliojulikana kama Communal Councils, na hii ilipelekea kuanzishwa kwa mipango ya kijamii iliyojulikana kama Bolovarian Missions iliyopanua upatikanaji wa chakula, nyumba, huduma za afya na elimu. 

Venezuela ilipata faida kubwa ya mafuta katikati ya miaka ya 2000, na kulikuwa na mabadiliko katika hali duni ya maisha, elimu, uwiano wa kipato na ubora wa maisha kwa ujumla kati ya 2003 na 2007. 

Kufikia mwisho wa urais wa Chavez mwanzoni mwa 2010, sera za uchumi zilizowekwa na serikali kama kubana matumizi na kudhibiti bei kulidhihirika hakuwezi kuendesha serikali wakati uchumi wa Venezuela ulikuwa unayumba, umasikini, bei za bidhaa zilipanda na mzunguko wa pesa ulipungua. 

Hii ilipelekea kiwango cha mauaji katika nchi kupanda, rushwa iliendelea katika idara za serikali mpaka polisi. Mfumo wake wa kuwezesha na kujitangaza kweke pia kulileta shida.

Kimataifa, Chavez alijijengea taswira kama mfuata mfumo wa Marxist na Lenini ambao Fidel na Raul Castro wa Cuba waliufuata, pia serikali ya Evo Morales (Bolivia), Rafael Correa (Ecuador) na Daniel Ortega (Nicaragua). Urais wake ulionekana kama ujamaa uliokwenda na wakati "pink tine" uliyosafisha Latin America.

Hugo alieleza sera zake kama za kupinga ubeberu, alionekana kama mtu mashuhuri aliyepinga sera za nje ya nje ya siasa za Marekani kwa sauti na upinzani wa hali ya juu. 

Aliunga mkono mfumo wa uchumi kumilikiwa na serikali. Alieleza kuwa yeye ni mfuata ujamaa na aliungwa mkuono na Latin American and Carribiean Cooperation, yeye alikuwa dhana ya kuunda umoja wa kanda ya Union of South American for the Americans, Bank of the South na pia television ya TeleSUR. Mawazo haya yalipelekea style ya Chavismo ambayo ni mfumo wa siasa ulioshirikisha Bolivia na ujamaa wa karne ya 21.

0 Comments:

Post a Comment