Thursday, March 19, 2020

RCL 2020: Muheza United ya Tanga

Ligi ya Mabingwa mikoa (RCL) ni miongoni mwa mashindano ya soka yanayosimamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). 

Kutokana na janga la dunia la virusi vya Covid-19 mashindano mbalimbali yanayosimamiwa na TFF yamesimama kwa agizo kutoka serikalini ili kuepusha maambukizi zaidi ya virusi hivyo. 

Hata hivyo kwa mechi chache zilizochezwa tunakuleteza timu moja moja katika Kundi B ambalo lilipangiwa kuchezwa katika Uwanja wa Ushirika, mjini Moshi, Kilimanjaro. 

Timu zilizokuwepo kwenye kundi hilo ni Cable SC (Arusha), Muheza United (Tanga), Mbuyuni Market (Kilimanjaro), Nyamongo FC (Mara), Mweta FC (Mwanza), Huduma (Dar es Salaam) na Babati Shooting Star (Manyara).

Mashindano hayo yalianza Machi 14, 2020 lakini yalisimamishwa Machi 17, 2020 ikiwa ni mitanange sita tu iliyochezwa kutokana na kitisho hicho cha Covid-19.

TFF ilitoa taarifa yake kuwa mashindano yake yatasiamama kwa siku 30 kupisha wasiwasi uliopo na kwamba baada ya siku hizo kuna uwezekano mkubwa wa timu kutocheza na mashabiki.

Ifuatayo ni timu ya Muheza United FC katika PICHA.

Muheza United lineup
Ally Mattaka, Awadhi Thomas, Ibrahimu Salimu, Abduli Mngoya, Adamu Rajabu, Ramadhani Omary, Emmanueli Haule, Kondo Shaibu, Issa Nassoro, Ramadhani Msumi.


Wa Akiba; John Anderson, Shabani James, Thomas Kabassa, Iddi Abdallah, Hussein Ally, Seif Sengao, Chelangwa Sultani.


STORY & PHOTO BY: Jabir Johnson
EMAIL: jabirjohnson2020@gmail.com
DATE: Machi 19, 2020



Ally Mattaka (Muheza United)

Nahodha wa Muheza United Abdul Mngoya (kushoto) akipambana na Hafidhi Mmbaga (kulia) wa Mbuyuni Market.







Ramadhani Omary (kulia) wa Muheza United akijaribu kumzuia mshambuliaji wa Mbuyuni Market Joramu Maingu. 





Ramadhani Omary akichuana vikali na Hafidh Mmbaga 

Joramu Maingu (17) wa Mbuyuni Market akionyesha kadi ya njao baada ya kumchezea rafu Ally Mataka wa Muheza United

Wachezaji wa Muheza United wakimwangalia mlinda mlango wao Ally Mattaka baada ya kuchezwa faulo na Joram Maingu katika mchezo dhidi ya Mbuyuni Market Machi 14, 2020 katika Uwanja wa Ushirika.




































Wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi la Muheza United wakifurahi baada ya ushindi dhidi ya Nyamongo FC Machi 17, 2020

0 Comments:

Post a Comment