Mkurugenzi
wa Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika CDC John Nkengasong
amesema, idadi ya kesi za maambukizi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na
virusi vipya vya korona (COVID-19) imepita 100 na mtu mmoja amefariki kutokana
na maambukizi hayo.
Nkengasong
amesema, kituo hicho kimepeleka wataalam 6 katika nchi za Nigeria na Cameroon
kusaidia kupambana na virusi hivyo, na mpaka sasa, nchi 43 za Afrika zina uwezo
wa kupima virusi hivyo.
Nkengasong
pia amesema, kituo hicho kinashirikiana na Shirika la Afya Duniani kutoa vifaa
vya upimaji wa virusi hivyo kwa nchi za Afrika na kuharakisha kununua vifaa vya
kupima joto ya mwili na vifaa vingine vya matibabu.
0 Comments:
Post a Comment