Mwanamuziki
wa reggae Keith Anderson maarufu Bob Andy amefariki dunia akiwa na umri wa
miaka 75 kutokana na kuugua kwa maradhi ya kansa.
Nyota
huyo amefariki dunia nyumbani kwake Stony Hill, St. Andrew jijini Kingston huko
Jamaica baada ya kupambana na Saratani kwa muda mrefu.
Mwanzilishi
huyo wa kundi The Paragons alichukuliwa kuwa miongoni mwa waandishi wa muziki
huo wenye ushawishi mkubwa ulimwenguni. Haikutosha kutoa nyimbo kali kwa sauti
yenye kuvutia kama I've Got to Go Back Home, Feeling Soul or Too Experienced
bali Bob Andy alionyesha uwezo mkubwa kwa nyimbo kali kama I Don't Want To See You Cry for Ken Boothe na ile ya Feel
Like Jumping for Marcia
Griffiths.
Baadaye
alikuja kupata umaarufu mkubwa pale walipoungana wawili Bob na Marcia kwa ajili
ya kulimata soko la kimataifa na wakafanikiwa kufanya hivyo mika ile ya 1970,
nyimbo kama Young, Gifted And Black or Pied Piper zilijidhihirisha wazi
kuwa Bob Andy alikuwa na kipaji kikubwa mno katika medani ya muziki wa reggae.
Baada
ya Marcia kuondoka na kwenda zake kuungana na I-Threes, Bob Andy aligeukia
kategori ya kucheza na kuigiza. Alifanya hivyo
alipoigiza akitumia jina la Luke katika filamu ya Children of Babylon
mnamo mwaka 1980 pia alitumia jina la Raisen
katika filamu ya The Mighty Quinn mnamo mwaka 1989.
Hakuacha
kazi yake ya muziki baada ya hapo alikwenda zake London na baadaye Miam ambako
alifanya kazi kama prodyuza kabla ya kuachia albamu ya Hangin Tough mnamo mwaka
1997.
Ziara
mbalimbali za muziki zilimfuata mkongwe huyo pale alipotua jijini Addis Ababa
huko Ethiopia wakati wa kumbukizi ya miaka 60 ya kuzaliwa kwa Bob Marley mnamo mwaka 2005.
Mwaka
mmoja baadaye alitunukiwa tuzo ya Kimataifa ya CD (Order of Distiction), kutokana
na mchango wake katika medani ya muziki wa Jamaica.
Kifo chake kimeushtua
ulimwengu ambapo Marcia Griffiths kupitia gazeti la Jamaica Obsever alikaririwa
akisema, “ Amefariki asubuhi hii ya saa 8:00 a.m…..(…) Jana nilifanya naye
mawasiliano kwa njia ya video.”
Ulimwengu wa reggae ulitoa salamu za rambirambi kutokana na kifo hicho.
Boby Andy alizaliwa Oktoba 28, 1944 Kingston Jamaica
Boby Andy alizaliwa Oktoba 28, 1944 Kingston Jamaica
Buju Banton:
“Nitakukosa sana rafiki yangu. Asante
sana kwa masomo kuhusu maisha.”
Clinton Fearon:
“Kaka yangu Bob Andy amefariki dunia. Alikuwa moja ya watunzi wa nyimbo
niliovutiwa nao, alikuwa na ushawishi mkubwa katika utunzi wangu. Ninakumbuka
nilikutana naye muda mfupi nchini Jamaica wakati nilizuru Kingston. Wakati ule
alikuwa akiishi na Marcia Griffiths. R.I.P brendin.”
David Rodigan:
“ Nimejawa na huzuni kubwa kutokana na kuondokea na Bob Andy asubuhi hii akiwa
nyumbani kwake Kingston, hakika alikuwa nembo ya muziki wa Jamaica na rafiki
yangu kipenzi ambaye ninajivunia kufahamiana naye miaka 35 iliyopita. Hakika
alikuwa mahiri katika uimbaji na utunzi wa zama zote sijawahi kuuona hapa
duniani. Katika albamu yake ya ‘Songbook’ pekee ni ushuhuda ambao umetoa
mchango mkubwa katika muziki na utu. Ulale mahali pema peponi hakuna maumivu
sasa. Rambirambi zangu kwa watoto na wote waliompenda.”
0 Comments:
Post a Comment