Mkutano wa 19 wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajia kuanza leo Machi 31 jijini Dodoma
huku Spika wa Bunge Job Ndugai akitoa utaratibu maalum utakaotumika tofauti na
ilivyozoeleka ili kujikinga na virusi vya ugonjwa wa Corona.
Moja ya hatua zilizochukuliwa awali ni kusitisha makundi ya wageni
wanaokwenda bungeni kujifunza namna bunge linavyoendesha shughuli zake Ndugai amesema kati ya wabunge wote, wabunge 150
hamsini ndiyo wataruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge ili kupunguza
msongamano.
Mkutano wa 19 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maalum
kwa ajili ya bajeti kuu ya serikali unatarajiwa kukamilika Juni 31 mwaka huu.
0 Comments:
Post a Comment