Tuesday, March 3, 2020

Unaikumbuka siku ambayo Pellegrini alikaribishwa kwa kichapo Bernabeu?

Machi 3, 2011 Real Madrid ilimpokea kwa staili kocha wake wa zamani katika dimba la Santiago Bernabeu kwa kuizabua timu yake kwa mabao 7-0.

Manuel Pellegrini aliiongoza Real Madrid kutoka Juni 2009 kwa msimu mmoja tu,  wakati akiinoa miamba hiyo ndipo alipofanikiwa kuwaleta wachezaji bora zaidi ambao walifanya ujio wao kuwa wa pili kwa kuwa ghali katika kikosi. 

Ricardo Kaka, Cristiano Ronaldo, Xabi Alonso, na  Karim Benzema waliletwa na kocha Pellegrini kwa ada ya pauni milioni 200.

Baada ya msimu mmoja Pellegrini alifungashiwa virago baada ya kushika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi ndipo walipomtimua ili waweze kumchukua Jose Mourinho

Novemba 2010 alisaini mkataba wa kuinoa Malaga kwa miaka mitatu.

Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kucheza na waajiri wake wa zamani.

Ilikuwa ni hatari kwani Ronaldo alifunga hat trick na mawili yalifungwa na Benzema. Angel di Maria na Marcelo waliongeza kila mmoja.

Hadi kipenga cha mwisho Malaga walikuwa wamesalia tisa uwanjani mmojawapo akiumia baada ya Pellegrini kumaliza wachezaji wa akiba na mmoja alitolewa kwa kadi nyekundu.

Mchezo huo uliwapeleka Malaga mpaka nafasi ya 19 ya msimamo lakini mwishoni mwa msimu walimaliza katika nafasi ya 11.

0 Comments:

Post a Comment