Monday, March 16, 2020

Unaikumbuka siku Ofisi za FC Barcelona zilipopigwa na bomu la Mussolini?

Machi 16, 1938 bomu lilipiga ofisi za klabu ya Barcelona wakati wa uvamizi wa Italia katika taifa hilo. Uvamizi huo ulifanywa na jeshi la Anga la Italia wakati huo ikitawaliwa na Fashisti Bennito Mussolini. 

Pia tukio hilo lilifanyika ikiwa ni miezi mitatu kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia. Kikosi cha Anga cha Italia (LAF) kilifanya uvamizi huo ili kumuunga mkono Francisco Franco dhidi ya wazaleno wa Katalunya waliokuwa wakitaka jimbo hilo lijitenge na utawala wa Franco. 

Barcelona ilikuwa ndio kitovu kikuu cha wazalendo hao wakipanga mipango  yao kwa ajili ya kupinga utawala wa Franco. 

Wakati huo Adolf Hitler wa Ujerumani  alikuwa ameungana na Mussolini. 
Wawili hao walikuwa wamempa msaada wa askari na vifaa Franco. 

Msaada wa jeshi la angani ulikuwa miongoni mwa misaada kwa Franco. Baada ya uvamizi huo miezi michache baadaye Katalunya iliangukia mikononi mwa wazalendo hao ambao walikuja na shikinizo jingine la kung'oa alama za Uhuru wa jimbo hilo. 

Barcelona ililazimishwa kuondoa bendera ya Katalunya. Pia Barcelona ililazimishwa kuondokana na jina la Football Club Bacelona na kuwa Club de Futbol Barcelona. 

Waungaji mkono wa mapizuzi hayo waliendeea  kuimba nyimbo wakitaka klabu ya Barcelona iwe ni nembo ya utaifa. 

Awali klabu hiyo ilikuwa haipewi kipaumbele na utawala wa taifa hilo kwani Franco aliipendelea zaid Real Madrid.  

Mnamo mwaka 1974 baada ya Franco kutangaza kwamba afya yake inazorota hali iliyomfanya  aachie ngazi kama mkuu wa taifa hilo, Barcelona ilirudisha bendera ya Kikatalunya katika nembo ya jimbo hilo. 

Pia walichukua jina la Futbol Club Barcelona  ambalo linatumika hadi sasa FC Barcelona.   

  

0 Comments:

Post a Comment