Monday, March 30, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Mama wa Malkia Elizabeth II ni nani?



Machi 30, 2002; Alifariki dunia Mama wa Malkia Elizabeth II. Jina lake halisi ni Elizabeth Angela Marguerite Bowes-Lyon
Huyu alikuwa ni mke wa mfalme George VI ambaye ni mama wa Malkia Elizabeth II na Princess Margaret wa Countess ya Snowdon. 

Huyu alikuwa ni Malkia wa Uingereza tangu alipotwaa mwaka 1936 hadi 1952 na kuanzia hapo alianza kuitwa mama wa Malkia Elizabeth. 
Mwaka 1952 alikabidhi taji la umalkia kwa binti yake na hiyo ndio sababu ya kuanza kuitwa jina hilo ili kuondoa mkanganyiko na jina la binti yake ambaye ni Malkia Elizabeth II. Mama wa Malkia Elizabeth wa pili alikuwa Malkia wa mwisho wa India. 

Alizaliwa katika familia ya kifalme ya Uingereza na alikuja kushika wadhifa huo alipoolewa mwaka 1923 pale Duke wa York na mtoto wa pili wa Mfalme George V na Malkia Mary. 

Mnamo mwaka 1936 mumewe hakutarajiwa kuwa Mfalme lakini alifikia hapo baada ya kaka yake Edward VIII kuondolewa katika nafasi hiyo kwani alikiuka amri ya kifalme pale alipomwoa mtalaka wa Kimarekani Wallis Simpson. 

Hivyo Elizabeth alikuwa Malkia. Enzi za utawala wake alishirikiana na mumewe kwenda katika ziara za usuluhishi wa kidiplomasia huko Ufaransa na Amerika ya Kaskazini ikiwa ni kabla ya kuanza kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka 1939. 

Wakati wa vita hiyo Malkia Elizabeth alionyesha ukomavu na asiyeshindwa kwani alisimama katika hadhira ya Waingereza na kutoa hutuba nyingi za matumaini. 

Baada ya vita, hali ya mumewe ilidhoofu na aliachwa mjane akiwa na umri wa miaka 51 na binti yake ambaye alikuwa na umri wa miaka 25 ambaye ndiye malkia wa sasa ambaye anachukuliwa kushika wadhifa huo kwa muda mrefu alipokea taji hilo. Baaada kifo cha Malkia Mary mnamo mwaka 1953, Elizabeth alichukuliwa kuwa msimamizi wa familia ya kifalme. 

Alikuwa imara katika hadhira hata kabla ya kifo chake. Akiwa na miaka 101 na siku 238 aliaga dunia ikiwa ni miezi saba baada ya kifo cha binti yake mdogo Princess Margaret. 

Malkia wa sasa alizaliwa kwa jina la Elizabeth Alexandra Mary Windsor mjini London tarehe 21 Aprili 1926 kama mtoto wa kwanza wa mfalme George VI wa Uingereza na Elizabeth Bowes-Lyon.
Malkia Elizabeth II ni mkuu wa Jumuiya ya Madola yeye ni pia mkuu wa dola wa nchi za Antigua na Barbuda, Australia, Bahamas, Barbados, Belize, Canada, Grenada, Jamaica, New Zealand, New Papua Guinea, Saint Kitts na Nevis, Saint Lucia, Saint Vincent, Visiwa vya Solomon, Tuvalu, Ufalme wa Muungano wa Uingereza na Ireland ya Kaskazini. 

Alipokea taji katika ibada rasmi tarehe 2 Juni 1953 kwenye kanisa la Westminster Abbey. Katika nchi zote anaposhika cheo hana mamlaka ya kiserikali anatawala kama mfalme wa kikatiba katika muundo wa serikali ya kibunge.



0 Comments:

Post a Comment