Machi 28, 1969 alifariki dunia mwanasiasa na mwanajeshi wa zamani wa Marekani Dwight D. Eisenhower. Eisenhower alishika wadhifa wa kuwa Rais wa 34 wa taifa hilo kutoka mwaka 1953 hadi 1961.
Enzi za utawala wake wengi walipendelea kumwita Ike (Aik). Baada ya kustaafu, Eisenhower alikaa pamoja na mke wake katika mji wa Gettysburg, Pennsylvania.
Alifariki dunia hospitalini baada ya kupatwa na mshtuko la moyo. Alifariki dunia asubuhi ya siku hiyo katika Hospitali ya Kijeshi ya Walter Reed jijini Washington akiwa na umri wa miaka 78.
Siku iliyofuata mwili wake ulipelekwa katika Kanisa la Bethlehem ambako ulikaa saa 28 kabla ya kupelekwa katika makao makuu ya Ikulu ya Marekani ya Capitol ambako ulilazwa katika viunga vya Capitol Rotunda Machi 30-31.
Mnamo Machi 31 ibada ya mazishi ilifanyika katika Kanisa la Kitaifa jijini Washington ambapo Rais wa wakati huo na mkewe Richard Nixon walihudhuria.
Pia katika ibada hiyo alikuwapo Rais wa zamani Lyndon Johnson. Wageni 2,000 walialikwa kuhudhuria ibada hiyo akiwamo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati huo U Thant na viongozi wengine 10 wa serikali akiwa Rais wa Ufaransa wakati huo Charles de Gaulle ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipozuru mazishi ya Rais John F. Kennedy.
Pia alihudhuria Shah wa Iran. Kwa wakati huo Gaulle na Mfalme Baudouin wa Ubelgiji walikuwa viongozi wanaojulikana sana.
Eisenhower alizaliwa Oktoba 14, 1890 akiwa mtoto wa tatu wa David na Ida Eisenhower katika mji wa Denison, Texas. Watoto wote saba walikuwa wavulana, majina yao: Arthur, Edgar, Dwight, Roy, Paul (aliyefariki utotoni na dondakoo), Earl, na Milton. Kabla Dwight hajafikisha umri wa mwaka mmoja, wazazi wake walihamia mji wa Abilene, Kansas, ambapo alilelewa na kuhitimu shule. Baada ya kufanya kazi mbalimbali za mikono, alifaulu mtihani wa kuingia chuo cha kijeshi cha Westpoint ambapo alihitimu mwaka wa 1915.
Julai 1, 1916, alifunga ndoa na Mamie Geneva Doud. Mtoto wao wa kwanza alizaliwa Septemba 23, 1917, jina lake Doud Dwight Eisenhower lakini aliitwa Icky Alifariki na homa ya vipele vyekundu (dondakoo) Januari 2, 1921, akiwa na miaka mitatu tu. Mtoto wa pili, John Sheldon Eisenhower, alizaliwa mwaka wa 1922.
Eisenhower alihamishwa kikazi mahali mbalimbali siyo Marekani tu lakini pia nje, k.m. Panama na Ufaransa.
Mara nyingi alifanya kazi ya ofisi ingawa alipendelea kazi yake ya kijeshi. Nafasi yake alifika wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Kuanzia mwaka wa 1942, Eisenhower alikuwa kamanda wa Jeshi, kwanza upande wa Afrika Kaskazini, akiwa na makao makuu mjini Algiers, halafu aliongoza uvamizi wa Italia, na mwishoni alitayarisha uvamizi wa Normandy Juni 5, 1944.
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia alikuwa jenerali mkuu aliyeongoza uvamizi wa Normandy Juni 5, 1944. Akiwa Rais makamu wake alikuwa Richard Nixon.
Baada ya vita alikuwa kamanda mkuu wa NATO. Watu wengi wa Chama cha Republican walimpendelea agombee urais mwaka wa 1952, yeye lakini hakutaka kuingia katika mambo ya siasa.
Hata hivyo alipita na kuwa mgombea wa Repulican. Baada ya kumshinda Adlai Stevenson III, Eisenhower alikuwa Rais wa Marekani kwa awamu mbili hadi 1961.
Wakati wa urais wake, vita ya Korea ilikomeshwa. Pia, siasa ya Marekani iliathiriwa na mawazo dhidi ya Wakomunisti yaliyotekelezwa na Joseph McCarthy.
Baada ya kustaafu, Eisenhower alikaa pamoja na mke wake katika mji wa Gettysburg, Pennsylvania. Tarehe 28 Machi 1969, alifariki hospitalini baada ya kupatwa na shtuko la moyo.
0 Comments:
Post a Comment