Machi 2, 2008 Iran ilihitimisha safari ndefu ya kutafuta kocha wa kuiongoza timu ya soka ya taifa hilo kwa kupata meneja mpya.
Hata hivyo hatua ya kumpata kocha mpya iliwastaajabisha wengi baada ya kumteua mfungaji wa zama zote wa kimataifa wa taifa hilo Ali Daei.
Licha ya kwamba Daei alisimamia mechi 24 tu lakini yumo katika orodha ya makocha waliokaa muda mrefu kuiongoza timu ya taifa hilo.
Enzi za uchezaji wake Daei alifunga mabao 109 katika timu ya taifa ya Iran aliyohudumu nayo kutoka mwaka 1993 hadi 2006.
Kumpata Daei ilikuwa baada ya harakati muda mrefu baada ya kutimuliwa kwa Branko Ivankovic aliyesimamia miamba hiyo kwa mechi 42 akishinda mechi 29.
Japokuwa raia huyo wa Croatia alikuwa kipenzi cha wapenzi na mashabiki wa soka wa Iran lakini halikuwa chaguo la serikali ambayo ilikuwa ikitaka raia wa Iran ndiyo awe msimamizi wa timu hiyo ikitanguliza zaidi kocha mzawa.
Baada ya Kombe la Dunia mnamo mwaka 2006 hadi ujio wa Daei makocha watatu wazawa walishika nafasi hiyo.
Wakati anachukua mikoba hiyo ya kuisimamia timu ya taifa ya Iran alikuwa na kibarua katika klabu ya Saipa FC ambapo alipewa majukumu yote mawili ya kusimamia timu ya taifa na kibarua chake kiweze kuendelea.
Katika ufungaji timu ya taifa ya Iran ilikuwa changamoto kubwa hali iliyosababisha kushindwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia la mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.
Changamoto hiyo ilimfanya aondolewa kuinoa miamba hiyo ya Asia baada ya mwaka mmoka licha ya ushindi wa mechi 16, sare 6 katika mechi 25.
Ushindi huo ulimpa nafasi ya kuwa bora kwa asilimia 64 ya makocha wazawa waliowahi kusimamia mechi zaidi ya 10.
Akiwa mchezaji aliwahi kucheza nchini Ujerumani kwa miaka sita kutoka mwaka 1997 hadi 2003 akiwa na Hertha Berlin, Bayern Munich na Arminia Bielefeld
0 Comments:
Post a Comment