Thursday, October 10, 2019

Binti wa miaka 14 apandishwa kizimbani kwa kujeruhi mtoto mwenzake


Binti wa miaka 14 nchini Botswana amepandishwa kizimbani kwa tuhuma kumjeruhi mtoto mwenzake kwa kumchoma kisu ambaye alihisi kuwa alihusika na mauaji ya bibi yake kwa kisu. 

Mahakama ya Serowe iliyopo katika jamii ya Bamangwato inaendelea kusikiliza kuhusu mashtaka hayo. 

Imedaiwa mahakama hapo kuwa bibi wa binti huyo aliuawa Juni mwaka huu. Binti huyo alimchoma kisu  kijana huyo ambaye ana umri wa miaka 18 nje ya mahakama wakati kesi kuhusu muuaji ilipokuwa ikiendelea. 

Akizungumza na vyombo vya habari Kamishna wa Jeshi la Polisi wa Kituo cha Serowe Poloko Oteng amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba kijana aliyechoma kisu alikimbizwa katika Hospitali ya Sekgoma Memorial kwa ajili huduma zaidi. 

Oteng amesema wanasubiri ripoti ya daktari kuhusu mhanga huyo. Hata hivyo ameweka bayana kuwa binti huyo wa miaka 14 ataadhibiwa kwa kutenda kinyume cha sheria. 

Aidha mtuhumiwa wa mauaji ya bibi yake yupo nje kwa dhamana huku binti huyo akiendelea kushikilia na Polisi na kwamba atapandishwa tena kizimbani baada ya uchunguzi. 

Wakati huo huo Jeshi la Polisi nchini humo linamshikilia kijana mmoja mwenye umri wa miaka 23 kutokana na mauaji ya kijana mwenzake wakati wakinywa pombe usiku kucha. 

Maofisa wa Polisi wa Letlhakane wamesema mtuhumiwa anafahamika kwa jina la Ookeditse Kabelo. 

Marehemu amefahamika kwa jina la Ofentse Nkhutswewho wote wakazi wa Central District. Imeelezwa kuwa siku ya tukio marehemu akiwa na rafiki yake walichukua redio na kwenda nayo wakinywa pombe wakisikiliza na kucheza muziki usiku mzima. 

Kamishna wa Polisi wa Kituo cha Letlkhane Michael Maphephu amesema mtuhumiwa alikwenda kumtembelea huko Mowana ambako marehemu alikuwa akikaa na kwamba uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atapandishwa kizimbani kujibu tuhuma za mauaji hayo.

0 Comments:

Post a Comment