Wednesday, October 30, 2019

Comoro: Mabadiliko ya Tabia Nchi, Vita ya Wote


Imeelezwa kuwa mapambano dhidi ya Mabadiliko ya Tabia Nchi sio vita ya mtu mmoja bali ni ya mataifa yote ulimwenguni. 

Wakizungumza katika Kongamano linaloendelea wa mabadiliko ya tabia nchini katika mji mkuu wa Komoro wa Moroni Vijana wanaoishi katika Bahari ya Hindi wamesema mapambano hayo yanatakiwa kufanyika na watu wote wanaoishi katika visiwa vilivyopo katika eneo hilo licha ya tofauti zilizopo. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mazingira ya Komoro Daniel Ali Bandar amesisitiza wajibu wa vijana katika mabadiliko ya tabia nchi.  

Muungano huo wa visiwafungu katika bahari ya Hindi umekuwa mwenyeji wa mkutano huo kwa mara ya pili tangu mwaka 2016. 

Kongamano hilo ni la 15 la Mabadiliko ya Tabia ya Nchi kwa Vijana waishio katika visiwafungu katika bahari ya Hindi. Katika siku tatu zote vijana hao wanajadili changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na suluhisho. 

Katika hotuba ya ufunguzi wa Kongamano Mratibu wa Mtandao wa Vijana wa Visiwafungu vya Bahari ya Hindi Ali Mohamed Moinabaraka amesema visiwafungu ndio viko kwenye ukanda wa kuathiriwa zaidi na mabadiliko hayo.


CHANZO: AL-WATWAN

0 Comments:

Post a Comment