Tuesday, October 29, 2019

MAKTABA YA JAIZMELA: Ellen Johnson SirLeaf (1938)



Ellen Johnson SirLeaf anafahamika zaidi kwa kuwa Rais wa taifa la Liberia kwa miaka 12 Kutoka Januari 16, 2006 hadi Januari 22, 2018 alipoachia madaraka kwa Mujibu wa Katiba na kukabidhi hatamu za uongozi kwa mchezaji wa zamani George Weah.

Sirleaf alizaliwa mwaka 1938 kwa baba Mliberia na mama mwenye asili ya Liberia Na Unerimani katika Jiji la kuu la kibiashara la Monrovia.

Aliolewa akiwa na umri wa miaka 17 na kufanikiwa kupata watoto wanne, ndoa yake ilivunjika mwaka 1961 kwa kumtuhumu mumewe James kwa kumnyanyasa.

Alijiendeleza kimasomo katika vyuo vikuu vya Marekani kikiwemo Chuo Kikuu cha Havard ambako alihitimu shahada ya uzamiri ya Masuala ya Utawala.

Mwaka 1980 aliikimbilia uhamishoni nchini Marekani baada ya kuikosoa Serikali ya Samwel Doe, mtawala aliyeingia madarakani kwa Mapinduzi.

Akiwa Nchini Marekani mwanamke huyo alifanya Kazi benki ya dunia. Mwaka 1981 hadi 1985 aliishi uhamishoni nchini Kenya akifanya Kazi benki ya Citibank.

Novemba 1985 alirejea Nchini mwake kushiriki Uchaguzi mkuu akilenga kuwania nafasi ya urais. Hata hivyo alikamatwa Na kuwekwa Katika kizuizi cha Nyumbani na kuhukumiwa kifungo Cha miaka kumi kwa mashtaka ya Uchochezi. Aliachiwa huru na kukimbilia Marekani akihofia kuuawa na vikosi vya Samwel Doe.

Mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia Ambapo mwaka 2005 alishinda uchaguzi mkuu dhidi ya mpinzani wake wa karibu mwanasoka wa zamani George Weah

Mwaka 2016 jarida Mashuhuri dunia la Time lilimtaja Sirleaf kushika nafasi ya 83 kwa Wanawake wenye ushawishi mkubwa Duniani.

Mwaka 2011 alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel kwa mchango wake wa kupigania haki za Wanawake Duniani.

0 Comments:

Post a Comment