Rais Filipe Nyusi wa
Msumbiji amewasili katika uwanja wa ndege wa Sochi nchini Russia leo asubuhi katika
ziara ya siku mbili katika Shirikisho hilo ukiwa ni mwaliko rasmi wa Rais
Vladimir Putin.
Taarifa ya Ikulu ya Msumbiji imesema kuwasili wa Nyusi kulipokelewa
na sherehe za kitamaduni zilizombatana na hotuba fupi akiwa hapo hapo uwanjani.
Katika ziara yake ya siku mbili nchini humo Nyusi atakutana na Rais Putin pia
na viongozi wengine wa Afrika ambao wapo nchini humo kwa ajili ya mkutano wa
Kiuchumi baina ya Russia na Afrika uliandaliwa kuimarisha uhusiano wa
kibiashara.
Rais Nyusi ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Mahusiano Jose
Pacheco, Waziri wa Usafirishaji na Mawasiliano Carlos Mesquita, Naibu Waziri wa
Madini na Nishati Augusto Fernando, Balozi wa Msumbiji nchini Russia Mario
Ngwenya.
Mkutano huo huko Sochi utafanyika kuanzia kesho Jumatano Oktoba 23
hadi 24 mwaka huu, ukibeba kauli mbiu ya; “Kwa amani, Usalama na Maendeleo.”
Nyusi atakutana na Putin hapo kesho.
0 Comments:
Post a Comment