Kwa
asili mwezi Oktoba ni mwezi wa nane katika mtiririko wa Kalenda ya Kirumi.
Asili ya neno Oktoba imetoka katika lugha ya kilatini ‘Octo’ ikiwa na maana ya ‘Nane’.
Baada ya kalenda za Julian na Gregori kuanza kutumika ukawa ni mwezi wa kumi.
Oktoba ni miongoni mwa miezi sita kati ya saba ambao una siku 31. Oktoba
ulikuwa ni mwezi wa nane wakati wa utawala wa kirumi wa Romulus mnamo mwaka 759
K.K Baadaye Oktoba ukawa mwezi wa kumi baada ya kuongeza miezi ya Januari na
Februari katika kalenda hiyo. Wakazi wa Saxons ambao walikuwa wakiishi katika pwani
ya bahari ya Kaskazini ambayo kwa sasa ni Ujerumani Oktoba walikuwa wakiuita ‘Wintirfyllith’
kutokana na kwamba mwezi huo ulikuwa na mbalamwezi na mwanzo wa baridi kali.
0 Comments:
Post a Comment