Ni taifa ambalo lipo
katikati ya taifa jingine ikiwa na maana limezungukwa pande zote na taifa ya
Afrika Kusini.
Lesotho ni miongoni mwa mataifa matatu ambayo ni huru yakiwa
yamezungukwa na taifa jingine na ni pekee nje ya Ulaya.
Lesotho ina eneo
linalochukua kilometa za mraba 30,000 likiwa na idadi ya takribani watu milioni
mbili tu. Idadi hiyo ya watu ni makadirio ya mwaka 2016 yanayoipa kuwa nchi ya
144 ulimwenguni kwa kuwa na idadi kubwa ya watu.
Mji mkuu ni Maseru. Hapo awali
Lesotho ilikuwa koloni la Waingereza ikiitwa Basutoland.
Ilipata uhuru wake
kutoka kwa Waingereza Oktoba 4, 1966. Kutokana na kuwa na mamlaka kamili
haikuwa vigumu kutambuliwa na Umoja wa
Mataifa, Jumuiya ya Madola na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Kwa kifupi ni kwamba jina Lesotho lina maana ya ‘Ardhi ya Watu wanaozungumza
Sesotho’. Wenyeji asilia wa taifa hilo ni Watu wa Jamii ya San ambao unaweza
kuwafahamu kupitia sanaa zao zilizopo katika mawe kwenye ukanda wa milimani.
Kuibuka kwa ufalme wa Moshoeshoe mwaka 1822
ambaye alikuwa mtoto wa Mokhachane aliyekuwa chifu mdogo kutoka ukoo wa
Bakoteli kulitengeneza ukoo mkubwa ambao ulianza kuonekana mwaka 1804.
Kati ya mwaka 1821 na 1823 wafuasi wa ukoo huo walianza kukaa katika milima ya
Butha-Buthe wakiungana na wapinzani wao wa zamani dhidi Lifaqane kutoka milki
ya Shaka Zulu kutoka mwaka 1818 hadi 1828.
Mataifa mbalimbali Uingereza,
Uholanzi na baadaye Ufaransa yalikuwa yakiliwania eneo hilo. Waingereza
walikamata eneo hilo kutoka mwaka 1869 hadi kupata uhuru kwao mwaka 1966. Kwa sasa
taifa hilo lina serikali yenye utawala wa kisheria wenye bunge lake.
Waziri
Mkuu wa Lesotho wa sasa ni Tom Thabane ambaye ni kiongozi mkuu wa serikali
mwenye mamlaka ya juu nchini humo.
Mfalme wa Lesotho ni Letsie III hana mamlaka
ya juu Zaidi ya kuhusika katika masuala machache yasiyo ya kisiasa. Baraza la
Seneti lina wajumbe 22 ambao ni machifu na wengine 11 wanaoteuliwa na Mfalme.
Machifu huchukua nafasi hizo kwa urithi hivyo wanapokeza kwa taratibu za ukoo
husika wa kichifu. Na wanaoteuliwa na mfalme hufanya kazi ya kumshauri Waziri
Mkuu katika baadhi ya masuala nchini humo.
Katiba ya Lesotho imechukua mfumo
huru wa masuala ya kimahakama ikianzia chini mpaka juu Mahakama za Kijadi hadi
mahakama ya Rufani. Lesotho imeundwa na wilaya 11 ambazo zinafanya uwepo wa
tarafa 80 nchini humo na kata 129.
Uchumi wa taifa hilo umejikita katika Kilimo,
Ufugaji, Manufacturing na uchimbaji wa madini. Walio wengi hujikita katika
kilimo. Madini ya almasi ndio yamekuwa yakichimbwa katika maeneo ya Letšeng,
Mothae, Liqhobong, na Kao.
Pesa inayotumika nchini humo ni Loti ambayo kwa
thamani ya kitanzani Loti Moja ni sawa na shilingi 155 ya Tanzania. Asilimia 95
ya raia wa taifa hilo ni wakristo.
Ripoti ya mwaka 2016 ilisema kuhusu muda wa
kuishi wa binadamu katika taifa hilo inakadiriwa kuwa ni miaka 51 kwa wanaume
na kwa wanawake ni miaka 55. Mwaka 2006 muda wa kuishi watu wa taifa la Lesotho
ulikuwa ni miaka 42.
0 Comments:
Post a Comment