Kuna msemo wa kiswahili
unaosema ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Kina dada wawili nchini
Swaziland wamefungiwa katika chumba kimoja kwa muda wa miaka nane sasa
wakisubiri wanaume wa kuwaoa kutoka kwa Bwana.
Gazeti la Times of Swaziland
limesema kina dada hao walifungiwa tangu mwaka 2012 wakiwa na umri wa takribani
miaka 20.
Hleziphi ambaye sasa ana umri wa miaka 34 na Ncobie Mphaphu mwenye
umri wa miaka 32 wanaishi katika chumba hicho katika eneo la Kashewula, Mnyamatsini.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo zinasema wanawake hao wawili bado ni
mabikira wakisubiri ufunuo kutoka kwa Bwana kuhusu kupata waume wa kuwaoa. Wanawake
hao ni waamini wa kanisa la Shembe Nazareth.
Gazeti la Times of Swaziland
limeandika kuwa kanisa hilo limechanganya tamaduni za Kizulu na Ukristo ndani
yake ambazo zimejikita katika Agano la Kale katika Biblia.
Mwanamke mmoja anayewatunza wanawake hao
wawili ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 50 amekaririwa akisema
hawaruhusiwa kutoka na kuonana na wanaume wanatakiwa kukaa humo wakiendelea
kuomba hadi Mungu atakapowafunulia.
CHANZO: TIMES OF SWAZILAND
0 Comments:
Post a Comment