Thursday, October 31, 2019

Kilimo uti wa mgongo wa Tanzania


Waziri Kilimo Japhet Hasunga akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira (kulia) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro (kushoto). Picha na Kija Elias, Moshi.

Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania. Kilimo huzalisha nusu ya uchumi wa nchi, robo tatu ya mazao yote yanayouzwa nje ya nchi, ni tegemezi la chakula na hutoa ajira ya karibu asilimia 80 ya Watanzania.

Licha ya sekta ya kilimo kuaajiri watu wengi hapa nchini, mchango wa Sekta hiyo  katika pato la taifa ni ndogo na watu wengi wanaojihusisha na kilimo  hasa katika maeneo ya vijijini bado ni masikini.

Sekta hii ya kilimo ni kubwa na ni muhimu kwa maendeleo ya taifa kwani karibu shughuli zote za kiuchumi zinazofanywa vijijini zinategemea sekta ya kilimo.

Ripoti ya Shirika la Kilimo Duniani (FAO) inasema mahitaji ya bidhaa za kilimo yanatarajiwa kukua kwa asilimia 15 katika kipindi cha muongo mmoja ujao huku, ukuaji wa uzalishaji wa bidhaa za kilimo ukitarajiwa kuongezeka kwa kasi zaidi na kusababisha mfumuko wa bei.

Aidha ripoti hiyo iliyotolewa mwezi Julai mwaka huu inatoa utafiti unaolenga mwelekeo wa miaka kumi ijayo katika soko la bidhaa za kilimo na samaki katika viwango vya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Katika ripoti hiyo inaelezwa kuwa miongoni mwa changamoto kubwa inayowakabili wakulima katika Mataifa yanayoendelea ikiwemo Tanzania ni pamoja na ukosefu wa masoko ya mazao yao ndani na nje ya nchi.

Katika miaka ya nyuma baadhi ya wakulima wa baadhi ya mazao kadhaa  wakiwemo wakulima wa zao la kahawa waliamua kuachana kabisa na uzalishaji wa mazao husika ikiwemo zao la Kahawa na korosho.

“Changamoto za wakulima kukosa masoko haziwaathiri wakulima pekee, bali hata serikali hivyo ni suala linalogusa pande zote, kwa sababu serikali nayo inategemea kupata mapato yake kutokana na usafirishaji wa mazao nje ya nchi.

0 Comments:

Post a Comment