Taifa hilo awali lilikuwa
likijulikana kwa jina la Malagasi. Ni taifa kisiwa kikiwa na takribani ya
kilometa 400 kutoka pwani ya Afrika Mashariki.
Ina ukubwa wa kilometa za mraba
592,800. Madagascar ni taifa kisiwa la pili kwa ukubwa duniani na kisiwa cha
nne kwa ukubwa ulimwenguni.
Taifa hilo linaundwa na visiwa vingine vidogo.
Kutokana na taarifa za kihistoria inaonyesha Madagascar ilitokana na
kugawanyika kwa Gondwanaland ikiwa miaka milioni 88 iliyopita.
Inaonyesha watu walianza kuishi miaka 10,000.
Makazi kabisa ya wanadamu yalianza miaka 350 K.K na 550 K.K Karne ya 9 B.K Wabantu
walihamia ukanda wa Msumbiji kutoka Afrika Mashariki. Mnamo mwaka 1897 kisiwa
cha Madagascar ilikuwa chini ya utawala wa Ufaransa hadi ilipopata uhuru mwaka
1960.
Madagascar imepitia vipindi vine vya mabadiliko ya katiba. Tangu mwaka
1992 taifa hilo liliweka misingi ya demokrasia inayofuata katiba na mji mkuu ni
Antananarivo. Ilijulikana sana kote ulimwenguni mwaka 2009 wakati wa kujiuzulu
kwa Rais Marc Ravalomanana na mwezi Machi mwaka huohuo Andry Rajoelina.
Mnamo Januari
2014 ilifahamika wakati pia wa ujio Hery Rajaonarimampianina aliyeshinda
uchaguzi wa mwaka 2013. Taifa hilo linazungumza Kifaransa na Kimalagasi na
ambazo lugha rasmi katika kisiwa hicho.
Chini ya utawala wa Ravolamanana
uwekezaji alioufanya ulilifanya taifa hilo kisiwa kukua kiuchumi lakini ulikuja
kushuka katika kipindi cha 2009-2013.
Madagascar ina takribani watu milioni
24.8
0 Comments:
Post a Comment