Wachimbaji wadogo wawili wamepoteza maisha
baada ya kufukiwa na kifusi katika eneo la machimbo yanayomilikiwa na Kampuni
ya Bitakwate Investiment katika Kijiji cha Buziba Kata ya Lwamgasa Wilaya ya
Geita.
Wachimbaji hao waliingia katika machimbo hayo ambayo yalikua
hayatumiki tena wakiwa na lengo la utafutaji wa dhahabu na ndipo walipokutwa na
mauti.
Wachimbaji hao wamekutwa na mauti usiku wa kuamkia oktoba 27
wamefahamika kuwa ni Jumanne Mgaya na Jovin Baraka.
Vifo hivi vimetokea zikiwa zimepita siku
27 tangu wachimbaji wengine wafukiwe katika Mgodi wa Imalanguzu huku mpaka leo
hii juhudi za kuwaokoa zikiendelea.
Ndugu Erasto Ndiyanabo ni
Mkurugenzi wa kampuni ya Bitakwate inayomiliki migodi huo amesema eneo hilo
lilikuwa limefungwa kutokana kutozalisha.
Mmoja ya wachimbaji Mathius
Pius amedai wachaji wanaamua kuingia maeneo hatarishi kutokana na ugumu wa
maisha walau wajipatie riziki.
Mkuu Mkoa wa Geita Mhandisi
Robert Gabriel ameagiza baadhi ya taasisi za serikali kufanya kazi kwa pamoja
kukagua na kuangalia athari zinazoweza kujitokeza hapo baadae katika maeneo
ambayo yamesitishwa shughuli za uchimbaji.
0 Comments:
Post a Comment