Thursday, October 10, 2019

MAKTABA YA JAIZMELA: George Hill Hodel ni nani?


Oktoba 10, 1907 alizaliwa daktari na muuaji raia wa Marekani George Hill Hodel. 

Daktari huyu alipatikana na makosa ya kumuua mwanadada Elizabeth Short ambaye alikuwa maarufu kwa jina la Black Dahlia. 

Hakuwahi kushtakiwa kwa mauaji hayo. Mwanadada huyo ambaye alikuwa mhudumu wa hoteli alitangazwa sana katika vyombo vya habari kutokana na mwili wake kukutwa ukiwa umeharibika sana. 

Black Dahlia alifariki dunia Januari 15, 1947 akiwa na umri wa miaka 22. Kilichosababisha kujulikana kwa muuaji ilikuwa ni mtoto wake ambaye alisema siku ya msiba wa baba yake kuwa ndiye muhusika mkuu wa mauaji ya mwanadada Black Dahlia. 

Hodel alifariki dunia Mei 16, 1999 akiwa na umri wa miaka 91. Mtoto wake aliyefahamika kwa jina la Steve Hodel aliwaambia maofisa wa polisi wa Los Angeles kuwa baba yake aliwahi kufanya mauaji mengine kadhaa. 

Kabla ya kesi ya Dahlia, pia alikuwa mtuhumiwa katika kifo cha katibu wake, Ruth Spaulding, lakini hakushtakiwa. Alishtakiwa pia kwa kumbaka binti yake mwenyewe, Tamar Hodel, lakini akahukumiwa kwa kosa hilo. 

Alikimbia nchi mara kadhaa, na kati ya mwaka 1950 na 1990. Inaelezwa alikimbia kwenda Ufilipino. Hodel alizaliwa Los Angeles, California kwa wazazi George Hodel Sr na Esther Hodel. Wazazi wake walikuwa na asili ya kiyahudi. 

Hodel alikuwa mtoto pekee wa kiume waliyemsomesha na kijana mwenye akili sana. Hodel alikuwa akipendelea kufanya muziki, alikuwa akipiga kinanda katika matamasha hapo hapo Los Angeles. 

Mtunzi wa nyimbo maarufu wakati huo Sergei Rachmaninoff aliwahi kusafiri hadi nyumbani kwa kina Hodel ili kumsikiliza kijana huyo akiimba. Alianza kusoma katika shule ya South Pasadena na alihitimu akiwa na miaka 15. 

Baada ya hapo alikwenda katika Chuo cha Teknolojia cha California (Caltech), Pasadena. Hata hivyo aliondoka chuoni hapo baada ya mwaka mmoja kutokana na kashfa ya ngono iliyomhusisha na mke wa Profesa. 

Hilo halikuwa kosa pekee kwa Hodel kwani alimtia ujauzito akiwa na malengo ya kuishi naye lakini mwanamke huyo alikataa. 

Mambo mengi ya daktari Hodel yalikuja kufahamika baada ya kifo chake. Likiwamo la kuumua kwa katibu muhtasi Ruth Splauding ili kuficha ukweli kuhusu upotevu wa fedha katika hospitali na kashfa za utoaji wa mimba ambazo zilikuwa kinyume na sheria.





0 Comments:

Post a Comment