Nigeria ni taifa lililopo Afrika
Magharibi linalopakana na Niger kwa upande Kaskazini, Chad kwa upande
Kaskazini-Mashariki, Cameroon kwa Mashariki na Benin kwa upande wa Magharibi.
Kwa upande wa kusini inapakana na Ghuba ya Guinea iliyopo katika bahari ya
Atlantiki. Taifa hilo linaundwa na Majimbo 36 na Mji Mkuu wa Shirikisho la
Majimbo hayo ambayo ni Abuja.
Katiba ya Nigeria inaitambua Nigeria kama taifa
la kidemokrasia lisilo na dini. Kwa sasa taifa hilo linaongozwa na Muhammadu Buhari
ambayo alishika mikoba hiyo tangu mwaka 2015.
Buhari alipokea kutoka kwa
Goodluck Jonathan. Nigeria imekuwa ikichukuliwa kuwa Mwamba ya Afrika kutokana
na kuwa na idadi kubwa ya watu kuliko Taifa lolote barani hapa. Ina takribani
watu milioni 186 ikiwa ni nchi ya saba duniani kwa kuwa na idadi ya watu.
Pia ni
nchi ya tatu baada ya China na India kwa kuwa na zaidi ya watu milioni 90 walio
chini ya umri wa miaka 18. Nigeria inachukuliwa kuwa ni taifa lenye makabila
akali ya 250 ambayo kwa kiasi kikubwa yakiongozwa na Wahausa, Wayoruba na
WaIgbo.
Zaidi ya lugha za kienyeji 500 zinazungumzwa nchini humo. Hata hivyo
Nigeria inaunganishwa na lugha ya Kiingereza cha Nigeria. Katika dini Nigeria
imekuwa ikimilikiwa na Wakristo na Waislamu.
Idadi kubwa wa Wakristo
inapatikana kusini mwa taifa hilo na waislamu wakiwa kaskazini mwa taifa hilo.
Kabla ya mwaka 1999 taifa hilo lilikuwa chini ya tawala za kidikteta. Mnamo
mwaka 2011 kulifanyika uchaguzi ambao ulimweka madarakani Rais Goodluck
Jonathan.
Uchaguzi huo unachukuliwa kuwa wa kwanza wa huru na wa haki na
kumpata rais kupitia sanduku la kura.
Imetayarishwa na Jabir Johnson…….Oktoba
3, 2019.
0 Comments:
Post a Comment