Ni taifa ambalo ni kisiwa
katika bahari ya Hindi, ikiwa ni umbali wa kilometa 2,000 kutoka Pwani ya Kusini
Mashariki ya bara la Afrika.
Taifa hili linaundwa na visiwa vya Mauritius,
Rodrigues, Agalega na St. Brandon. Visiwa vya Mauritius na Rodrigues vinaunda
kwa pamoja mkusanyiko wa visiwa vya Mascarene ambavyo vipo karibu na koloni la
Ufaransa la Reunion.
Mji mkuu wa taifa la Mauritius ni Port Louis ambao upo
katika kisiwa kikuu cha Mauritius.
Ukubwa wa taifa hilo ni kilometa za mraba
2,040. Mnamo mwaka 1598 Wadachi walichukua umiliki wa taifa hilo. Mnamo mwaka
1710 waliachia na ndipo Ufaransa ikaanza kuchukua umiliki wake mwaka 1715.
Baada ya Ufaransa kuchukua umiliki wa taifa hilo ilianza kuitwa kwa jina la
Isle de France.
Mkataba wa Paris
uliowakutanisha Ufaransa na Uingereza
mnamo Mei 30, 1814 uliwafanya Ufaransa kuchukua umiliki kamili wa taifa
hilo pamoja na Reunion. Awali Ushelisheli ilikuwa inatakiwa kuwa miongoni mwa
koloni la Uingereza ndani ya Mauritius lakini ikajitenga mnamo mwaka 1906.
Mamlaka ya Tromelin iliyaingiza mataifa hayo mawili katika mfarakano, kwamba
katika mkataba wa Paris St. Brandon, Chagos, Agalega na Tromelin hayakuingizwa
katika makubaliano hayo.
Mnamo mwaka 1965 miaka mitatu baada ya uhuru wa Mauritius,
Uingereza iliitenganisha Chagos Archipelago kutoka katika mamlaka ya Mauritius;
visiwa vya Aldabra, Farquahar na Desroches kutoka Ushelisheli ili kuunda kile
kinachoitwa Mamlaka ya Uingereza katika Bahari ya Hindi (BIOT).
Hata hivyo
mgogoro huo ulichukua miaka mingi ya kupata suluhu lakini Februari 2019 Mahakama
ya Haki ya Kimataifa iliamua kuwa Uingereza inapaswa kurudisha mamlaka ya
Chagos Archipelago katika taifa la Mauritius. Watu wanaoishi Mauritius ni
mchanganyiko katika kila kitu, katika lugha, katika utamaduni na katika dini.
Mfumo
wa Bunge la Taifa hilo ni ule wa Westminster. Pia taifa hilo lina kiwango cha
juu cha demokrasia, siasa na uhuru wa kiuchumi.
Mauritius imekuwa ikichukuliwa
kuwa juu katika Human Development Index. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia taifa
hilo lina uchumi wa juu-kati katika mapato.
Serikali ya taifa hilo imekuwa
ikijali masuala ya afya na elimu bure kwa kutoa usafiri bure kwa wanafunzi,
raia wa juu wa taifa hilo na wenye ulemavu. Mnamo mwaka 2019 Mauritius ilikuwa
katika kiwango cha juu cha usalama nan chi yenye usalama zaidi kwenye viwango
vya Global Peace Index.
Pia Mauritius imekuwa ikifahamika sana kutokana na uoto
wa mimea na viumbe mbalimbali. Na kwamba Mauritius imekuwa ndio makazi ya ndege
aina ya Dodo na aina nyingine. Kwa makadirio ya sense ya watu ya makazi yam
waka 2018 taifa hilo lina takribani watu milioni 1.2
Baada ya Rais mwanamke
Ameenah Gurib-Fakim kujiuzulu tangu mwaka 2016 taifa hilo limekuwa mikononi mwa
aliyekuwa makamu wa Rais Barlen Vyapoory.
Imetayarishwa na Jabir Johnson.......................Oktoba 28, 2019
0 Comments:
Post a Comment