Zimbabwe ni nchi ambayo ipo
Kusini mwa Afrika kati ya mto Zambezi na Limpopo. Zimbabe imepakana na Afrika
Kusini, Botswana, Zambia na Msumbiji. Mji Mkuu wa Zimbabwe ni Harare na mji
mkuu kwa ukubwa nchini humo ni Bulawayo.
Nchi hiyo ina takribani
milioni 16. Ina lugha zipatazo 16 zinazozungumzwa lakini Kiingereza , Kishona
na Kindebele ndizo ambazo mara nyingi zimekuwa zikitumika.
Tangu karne ya 11 eneo
ambalo kwa sasa linaitwa Zimbabwe limetawala na falme mbalimbali. Zimbabwe ilijipatia uhuru kutoka kwa
Waingereza mwaka 1980.
Taifa hilo lipo katika
jumuiya mbalimbali za Kimataifa, ambazo ni Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa
Afrika (AU), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na COMESA.
Pia Zimbabwe
imekuwa ikifahamika kwa jina la ‘Kito cha Thamani cha Afrika’, kutokana na
ukuaji wake. Hata hivyo huwezi kuizungumza Zimbabwe bila kumtaja kiongozi
maarufu wa taifa hilo aliyefariki dunia Septemba 6, 2019 nchini Singapore akiwa
na umri wa miaka 95.
Nchi za Magharibi zimekuwa
zikikosa utawala wake kutokana na tabia yake ya kutotii matakwa ya mataifa hayo
ambayo inatafsiriwa kama kiburi.
Mugabe aliondolewa madarakani Novemba 21, 2017
na kundi la Emmerson Mnangagwa ambaye baada ya uchaguzi wa Julai 30, 2018
alikuwa mwenyekiti wa ZANU-PF na Rais wa Taifa hilo kwa sasa.
Katika uchaguzi huo
Mnangagwa alipambana na kijana Nelson Chamisa ambaye anaongoza chama cha
upinzani cha MDC Alliance.
Zimbabwe ina majimbo 8 ambayo
ni Bulawayo, Harare, Manicaland, Mashonaland Central, Mashonaland East, Mashonaland
West, Masvingo, Matabeleland North, Matabeleland South na Midlands. Pia
Zimbabwe ina wilaya 59 na kata 1,200.
Katika uchumi wa taifa hilo
lililopo Kusini mwa bara la Afrika; madini, dhahabu na kilimo yamekuwa ni
kiungo kikubwa kinacholiingizia taifa hilo fedha za kigeni. Utalii pia ni
kiungo muhimu katika uchumi wa Zimbabwe.
0 Comments:
Post a Comment