Serikali ya Lesotho
imeongeza mkataba wa uchimbaji wa madini ya almasi kwa miaka 10 mingine na
kampuni la uchimbaji wa madini hayo la Letšeng.
CHANZO: LESOTHO TIMES
Kampuni kubwa la madini
nchini humo la Gem limetoa tangazo hilo kwamba mkataba mpya uliosainiwa na
serikali ulianza kufanya kazi tangu Okotba 3 mwaka huu.
Gem imesema mkataba huo
umeongeza mauzo kutoka asilimia 8 hadi 10 tangu uliposainiwa mwanzoni mwa mwezi
huu.
Kuongezwa kwa miaka katika
mkataba huo kutalifanya kampuni hilo kumaliza makubaliano hayo 2034 kutokana na
kwamba mkataba wa sasa wa uchimbaji utamalizika 2024.
Kuongezwa kwa mrahaba huo
kuongeza ufanisi katika maeneo mengi ambayo bunge la nchi hiyo lilikuwa
likinyoshea kidole cha lawama kampuni hilo kwamba kampuni hilo limekuwa
likilipa chini ya asilimia 10.
Gem Diamonds inamiliki
asilimia 70 ya uchimbaji huo huku serikali ikichukua asilimia 30 ya uchimbaji.
Soko la Hisa la London
(LSE) katika taarifa zake liliandika kuwa serikali ya Lesotho imerusha mkataba
wake na Gem Diamonds.
Mkurugenzi Mtendaji wa Gem
Clifford Elphick amesema kuongeza mkataba kutasaidia na kuchangia kwa kiasi
kikubwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa raia wa Lesotho.
CHANZO: LESOTHO TIMES
0 Comments:
Post a Comment