Takribani familia milioni
mbili nchini Angola zitanufaika na mpango wa kilimo wa 2019/2020 unaosimamiwa
na serikali ya nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Kilimo na Misitu wa
Angola António Francisco de Assis wakati wa uzinduzi wa Msimu wa Kilimo 2019/2020
uliofanyika Cahunda katika jimbo la Malanje Kaskazini juzi Jumatano
imesema matrekta 990 yanatarajiwa
kutolewa nchi nzima.
Familia milioni mbili zitafaidika na matreka hayo huku
zikisalia familia milioni 1.47 za wakulima nchini humo. Wizara hiyo imesema
utoaji wa matrekta hayo ni muhimu kwani utasaidia familia hizo za wakuliwa
katika msimu wa kilimo na kwamba jumla
ya hekta milioni 5.6 zinatalimwa kupitia matrekta hayo hivyo uzalishaji
utaongezeka.
Wakati huo huo taifa hilo limepanda katika viwango vya soka
vinavyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). Black Sables likiwa ni
jina la timu ya taifa hilo ipo nafasi ya 31 ikiwa miongoni mwa timu bota barani
Afrika. Senegal imeshika nafasi ya 20, Tunisia 29, Nigeria ya 35.
Hivyo kwa
viwango hivyo Angola ipo nafasi ya nne katika timu za Afrika. Cape Verde ipo nafasi ya 77 ikiwa miongoni mwa
timu bora katika ukanda wa mataifa yanayozungumza Kireno.
Brazili imeshika
nafasi ya tatu katika viwango hiyo. Ubelgiji imeshika nafasi ya kwanza katika
viwango hivyo vilivyotangazwa jana Alhamisi.
0 Comments:
Post a Comment