Afrika Kusini ni nchi kubwa
ya Afrika ya Kusini yenye wakazi takriban milioni 57.
Ni taifa pekee barani
Afrika ambali linatoka upande wa Kusini iliko bahari ya Atlantiki hadi Mashariki
iliko bahari ya Hindi. Ikichukua takribani kilometa 2,798.
Imepakana na
Namibia, Botswana, Zimbabwe, Msumbiji na Uswazi. Nchi nzima ya Lesotho iko
ndani ya eneo la Afrika Kusini.
Mji mkubwa ni Johannesburg. Majukumu ya mji
mkuu yamegawiwa kati ya miji mitatu: Cape Town ni makao ya Bunge, Pretoria ni
makao ya Serikali na Bloemfontein ni makao ya Mahakama Kuu.
Taifa hili
linatumia lugha rasmi 11, nazo ni: Kiafrikaans, Kiingereza, Kizulu, Kixhosa,
Kiswati, Kindebele, Kisotho cha Kusini, Kisotho cha Kaskazini, Kitsonga,
Kitswana na Kivenda. Chanzo cha Afrika Kusini ni kwamba Waholanzi walikaa
katika rasi ya Cape Town.
Huko kabila jipya la Makaburu lilijitokeza kati ya
walowezi Wazungu kutoka Uholanzi, Ufaransa na Ujerumani.
Lugha yao ilikuwa
Kiholanzi iliyoanza kuchukua maneno ya Kifaransa, Kiafrika na Kiingereza na
kuendelea kuwa lugha ya pekee Kiafrikaans. Karne za kwanza za koloni la
Kiholanzi watumwa kutoka Indonesia waliletwa kama wafanyakazi wa Waholanzi na
Makaburu.
Hao Waindonesia walikuwa chanzo cha jumuiya ya Uislamu kwenye rasi. Pia
machotara walitokea kutokana na kuzaliana kati ya Makaburu na wanawake Waafrika
na Waindonesia.
Sehemu ya machotara hao wameingia katika jumuiya ya Makaburu na
wengi wao wanapimwa kuwa na mababu Waafrika. Katika miaka ya baadaye ubaguzi wa
rangi uliongezeka na watoto machotara wa Wazungu na Waafrika mara nyingi
hawakukubalika; walianza kuishi kama kundi la pekee kati ya Waafrika na
Wazungu, nao ni chanzo cha hao walioitwa baadaye "Cape Coloreds".
Sehemu
kubwa ya eneo kaskazini kwa rasi ilikaliwa na makabila ya Waafrika.
Mnamo mwaka 1800 falme na milki zilianza
kutokea hapa. Mwanzo wa karne ya 19 ni hasa Wazulu chini ya Shaka Zulu
walioanza kuenea na kuwashambulia majirani katika vita vya Mfecane.
Vita hivyo
vilileta uharibifu mkubwa lakini vilisababisha pia kutokea kwa milki za Wasotho
na Watswana na wengine walioiga mitindo ya Wazulu na kujenga madola yenye uwezo
wa kijeshi.
Mwaka 1814 Koloni la Rasi lilitwaliwa na Waingereza na kuwa sehemu
ya Milki ya Uingereza.
Utawala wa Waingereza ulisababisha uhamisho wa nje wa
sehemu ya Makaburu waliotokana na Wazungu kutoka Uholanzi, Ufaransa na
Ujerumani; Makaburu hao walihama kwenda kaskazini wakaanzisha jamhuri ndogo
kati ya maeneo ya Waafrika ama kwa njia ya mapatano au kwa njia ya vita.
Kati ya miaka 1840 na 1850 Waingereza
waliwafuata Makaburu kwa kueneza maeneo yao hadi mto Oranje; waliteka jamhuri
ya Kikaburu ya Natalia na kuanzisha koloni jipya la Natal.
Jamhuri mbili za
Makaburu ziliweza kustawi kwa miaka kadhaa ambazo zilikuwa jamhuri ya Dola Huru
la Oranje upande wa kaskazini wa mto Oranje na jamhuri ya Transvaal (ilijiita
pia Jamhuri ya Kiafrika ya Kusini) upande wa kaskazini wa mto Vaal.
Yapo mengi
ya kuzungumza kwa taifa hili la Afrika Kusini lakini ni miongoni mwa mataifa
yenye watu wengi ulimwenguni likishika nafasi ya 24 takribani watu milioni 57
kwa makadirio ya mwaka 2018.
0 Comments:
Post a Comment