Oktoba
9, 1966 alizaliwa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza David Cameroon.
Waziri
Mkuu huyo aliiongoza Uingereza kuanzia mwaka 2010 hadi alipojiuzulu mwaka 2016.
Kabla ya hapo alikuwa mbunge wa Witney kati ya mwaka 2001 hadi 2016 na pia kiongozi
wa chama cha Conservative kutoka mwaka 2005 hadi 2016.
Enzi za utawala wake alifanya marekebisho makubwa ya sera za kiuchumi na kijamii za taifa hilo. Alijiuzulu na kumpisha Waziri Mkuu Theresa May ambaye naye amejiuzulu mwaka huu (2019) na nafasi yake kuchukuliwa na Boris Johnson.
Cameroon alizaliwa katika familia yenye uwezo wa juu wa maisha. Alizaliwa katika kitongoji cha Marylebone jijini London na kukulia Peasemore, Berkshire.
Alizaliwa na ndugu zake wengine kaka yake ni Alexander Cameroon (1963), dada zake wawili Tania Rachel (1965) na Clare Louise (1971). Cameroon alizaliwa kwa wazazi Ian Donald (1932-2010) na Mary Fleur (1934). Wazazi wake walifunga ndoa Oktoba 20, 1962. Cameroon alianza kusoma katika shule ya Heatherdown, pia chuo cha Eton na Brasenose zilizopo Oxford.
Mnamo mwaka 1988 aliingia katika Idara ya Utafiti ya Conservative aliyodumu nayo hadi mwaka 1993. Pia Cameroon aliwahi kuwa msaidizi wa Waziri Mkuu wa zamani wa Conservative John Major kabla hajaondoka mnamo mwaka 1994 na kwenda kufanya kazi na kampuni ya Mawasiliano ya Carlton.
Kimataifa Cameroon aliruhusu kuingilia kijeshi vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Libya na kuendesha operesheni nchini Iraki dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu (IS).

0 Comments:
Post a Comment