Wagombea 817 wa viti
mbalimbali nchini Mauritius wameandikishwa katika majimbo 21 nchini humo kwa
ajili ya uchaguzi ujao wa Novemba 7 mwaka huu.
Taarifa ya serikali ya Mauritius
imesema idadi ya wagombea mwaka huu imevunja rekodi tangu kuanza kufanyika kwa
uchaguzi nchini humo mwaka 1967. Vyama vitatu nchini humo vya MSM-ML, Ptr-PMSD
na MMM vimepeleka wagombea 60 katika majimbo hayo yakiwamo ya Rodrigues na
Agalega.
Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa wapiga kura waliondikishwa wamefikia
941,719 kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwaka huu nchini humo. Serikali ya taifa
hilo inaundwa na chama chenye wingi wa viti bungeni.
Kiongozi wa
chama kimojawapo atakayekuwa na wingi wa viti bungeni ndiye atakuwa Waziri Mkuu
na kuongoza serikali ya taifa hilo. Na wa pili katika kupata viti bungeni
atakuwa kambi ya upinzani katika serikali ya taifa hilo.
CHANZO: REPUBLIC OF MAURITIUS
0 Comments:
Post a Comment