Oktoba
26, 1947 alizaliwa mwanasheria na mwanasiasa mwanamke wa Marekani Hillary
Rodham Clinton. Kwa sasa ni seneta wa Jimbo la New York nchini Marekani. Jina
lake halisi ni Hillary Diane Rodham.
Ameolewa
na rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton. Wakati mumewe alipokuwa rais,
Hilary alipewa jina la mwanamke wa kwanza au mke wa rais wa Marekani. Alikuwa mwanamke
wa kwanza wa Arkansas kabla ya kuwa mwanamke wa Kwanza wa Marekani.
Alianza
kufanya kazi kama Seneta Januari 3, 2001. Hillary Clinton alikuwa mwanamke wa
kwanza kuwa seneta wa New York. Aliendelea kuwania tena kiti hicho cha Useneta
katika uchaguzi wa mwaka 2006, ambapo pia aliibuka mshindi.
Hillary Diane Rodham
alizaliwa mjini Chicago, Illinois. Jina la babake ni Hugh Rodham, Sr., na jina
la mamake ni Dorothy Emma Howell Rodham. Pia ana ndugu wa kiume wawili, Hugh na
Tony.
Alipata elimu yake katika
shule ya Maine East High School na Maine South High School. Alimaliza elimu
yake ya awali kunako mwaka wa 1965, na baada ya hapo akaenda kujiandikisha
katika chuo cha Wellesley, karibu na mji wa Boston.
Mnamo mwaka wa 1969, Rodham
alielekea Chuo cha Sheria, kilichokuwa kinamilikiwa na Yale. Baada ya hapo
akapata digrii yake ya ualimu wa sheria katika Chuo Kikuu cha Yale mnamo mwaka
wa 1973. Kisha akawa anafanya kazi ya kujitolea katika Kutuo cha Kufundishia
Watoto cha Yale, kilichokuwa kinajulikana kwa jina la Yale Child Study Center.
Wakati anafanya kazi kama
mwanachama wa kitengo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Arkansas, akaolewa na Bill
Clinton ambaye naye alikuwa akifanya kazi hiyohiyo aliyokuwa anafanya mkewe
katika Chuo Kukuu hicho.
Wote walifahamiana wakati wanasoma katika Chuo cha
Sheria cha Yale. Kwa pamoja wamebarikiwa kupata mtoto mmoja pekee aitwaye
Chelsea Clinton, aliyezaliwa Februari 27, 1980.
Hilary alikuwa miongoni mwa wagombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2008. Aligombea kupitia Chama
cha Demokrasia (kwa Kiingereza Democratic Party).
0 Comments:
Post a Comment