Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai. (1922-1999). |
Nchi ya Tanzania hii leo
imeadhimisha miaka 20 ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa taifa hilo Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere ambaye aliaga dunia Oktoba 14, 1999.
Imekuwa ni siku ya mapumziko, wakati huu ambapo wananchi
wameendelea kuyaenzi yale mazuri aliyowaachia hayati baba wa taifa hilo ambaye
wakati wa uhai wake alisisitiza suala la amani na Umoja miongoni mwa Watanzania
na bara la Afrika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania John Pombe Magufuli amekemea vikali suala la rushwa nchini humo na
kutaka wahusika wawachukulie hatua wale wanaopatikana na hatia.
Watanzania wengi
wanamkumbuka baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alifariki
Octoba 14, 1999 ikiwa ni miaka 120 leo. Watanzania wanamuenzi mwalimu kwa mengi,
lakini kuu ni ile falsafa yake ya umoja ambayo ilimpelekea kuunganisha
Tanganyika na Zanzibar.
Mwalimu Nyerere
anaheshimiwa na Watanzania wengi kwa uadilifu na moyo wake wa kutumikia kuliko
kutumikiwa.
Julius Nyerere alizaliwa
mwaka 1922 katika eneo la mashariki mwa Ziwa Victoria na aliyeishi katika
maisha ya kawaida, ambapo baba yake alikuwa kiongozi wa kabila ndogo.
Alianza shule akiwa na umri
wa miaka 12 na alisomea taaluma ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini
Uganda. Baada ya kufundisha kwa miaka mitatu alipata ufadhili wa kusomeshwa
katika Chuo Kikuu cha Edinburgh.
Alifundisha Kiingereza,
Kiswahili, na historia katika Chuo Kikuu cha jijini Dar es Salaam, na kutokana
na mwenendo wake aliochaguliwa kuwa mkuu wa shirika la Tanganyika African
Association.
0 Comments:
Post a Comment