Hayati
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 , katika kijiji cha
Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara.
Alikuwa moja
kati ya watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa
mtoto Nyerere alichunga mifugo ya babake; katika umri wa miaka 12, aliingia
shule akitembea kilomita 30 hadi katika shule ya msingi ya Mwisenge, iliyoko
Musoma Mjini.
Baada ya
kumaliza shule ya msingi aliendelea kusoma shule ya wamisionari Wakatoliki
iliyoko Tabora. Katika umri wa miaka 20, Nyerere alibatizwa akawa mkristo
Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake. kutokana na ujasiri na nia ya kuwa
mwelewa wa kila kitu ya Nyerere, Mapadre wa Kanisa katoliki wakaona akili yake
na nia yake nzuri ya kutaika kujifunza wakamsaidia kusoma kozi ya ualimu katika
Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945.
Akiwa katika
Chuo cha Makerere akaanzisha tawi la Umoja wa wanafunzi Watanganyika pia
akaamua kujihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA). Baada ya
kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya sekondari ya
Mtakatifu Maria (St.Mary´s), Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma
kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskoti / Uingereza akasoma Shahada ya
Uzamili ya historia na uchumi, kwa hatua hiyo Mwalimu alikuwa mtanzania wa
kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na mtanzania wa pili kupata
shahada ya elimu ya juu nje ya Tanzania.
Aliporejea
Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na
Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam, (siku hizi
Pugu Sekondari). Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika
African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa
mwanafunzi katika huo kikuu cha Makerere.
Mwaka 1954, alikibadilisha chama cha
TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho
kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU
kilikuwa tayari chama cha siasa kinachoongoza Tanganyika. Uwezo wa mwalimu
uliwashitua viongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere kuchagua kati ya siasa
na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua
na mwanasiasa kwa bahati mbaya.
Aliamua kujiuzulu
ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu
ili kuleta muungano katika mapigano ya uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU
katika Mkutano wa Baraza la udhamini (Trusteeship council) ya Umoja wa Mataifa
(UN) huko New York. Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha
Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu.
Ushirikiano mzuri aliouonyesha
aliyekuwa gavana wa wakati huo Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha
upatikanaji wa uhuru. Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na
kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960.
Mwaka 1961
Tanganyika ilipata uhuru wake na Desemba 9,1961 Nyerere alichaguliwa kuwa
waziri mkuu wa Tanganyika huru na mwaka mmoja baadae Nyerere alikuwa raisi wa
kwanza wa jamhuri ya Tanganyika.
Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika katika
muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania baada ya mapinduzi ya
Zanzibar mwaka 1964, yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin
Abdullah.
Hayati
Mwalimu Nyerere mnamo Februari 5, 1977, aliongoza chama cha TANU katika tendo
la kuungana na chama tawala cha Zanzibar ASP na kuanzisha chama kipya cha CCM
(Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake.
Nyerere
aliendelea kuongoza Taifa hadi 1985 alipong’atuka na kumwachia nafasi rais wa
awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi. Aliendelea kuongoza Chama cha CCM hadi 1990 na
kuwa na makini na mfuatiliaji huku akionya katika mambo kadhaa katika siasa ya
Tanzania hadi kifo chake. baada ya kustaafu kazi ya ukuu wan chi, Nyerere
alikaa muda mwingi kijijini kwake alikozaliwa Butiama akilima shamba lake la
mahindi.
Pamoja na
haya alianzisha taasisi yenye jina lake inayojulikana kama “Mwalimu Nyerere
Foundation, mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali wa vita
vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.
Mwishoni mwa
maisha yake Mwalimu aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama
Mwalimu alianza kujisikia vibaya mwezi Augost mwaka 1999, akaanza kupata
matibabu ya kila mara baadaya alihamishiwa katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas
huko Uingereza.
Oktoba 14,
1999 aliaga dunia katika hospitali hiyo ambapo madaktari walisema kuwa alikuwa akisumbuliwa
na kansa ya damu (leukemia).
Kitendo
kikubwa ambacho hakisahahuliki ambacho Mwalimu alikifanya na dunia inakumbuka
ni kuchanganya ardhi za Zanzibar na Tanganyika ambapo Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ulizaliwa rasmi na hadi leo upo.
Kujenga
umoja wa kitaifa na utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili,
kushinda ubaguzi wa rangi, kutetea usalama wa taifa katika vitani dhidi Nduli
Idi Amin Dada wa Uganda. watu walimuita mwalimu kuwa ni mwanamapinduzi wa
afrika, kiongoiz wa bara nzima kutokana na nia zake za kutaka kila Mwafrika
kuwa huru na kuwa na amani.
Mwalimu pia
alifanikiwa kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za kusini ya Afrika
kama; Zimbabwe {ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola
(MPLA) na Msumbiji (Frelimo)
Kitu ambacho
kilimuumiza mwalimu na kumfanya akose raha mara nyingi ni juu ya kutofanikiwa
kwa nia yake ysa kuanzisha siasa za Kijamaa. Siasa zake za ujamaa zilishindwa
baada ya mwaka 1976.
Baada ya
kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa za kijamaa na
kutoweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa ambazo yeye hakuwa muumini, Nyerere
kwa maamuzi yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais baada ya uchaguzi wa
mwaka 1985 na kumwachia usukani kwa Mwinyi aliyetawala kwa siasa za uchumi wa
soko huria.
Katika hali ya kukubali ukweli, Nyerere alitamka katika tafrija ya
kumwaga juu ya siasa yake kiuchumi “Nimefeli. Tukubali hivyo.” Alikosolewa pia
Kutokana na hali hiyo na kufikia yeye kukubali kushindwa Mwalimu Nyerere
analaumiwa kwa siasa zake za kiujamaa kuwa zilichelewesha maendeleo ya kiuchumi
wa Tanzania, Pamoja na kwamba hata leo kuna makundi ya watanzania kwa mtazamo
wao yanazitamani siasa hizo. Pia kuna makundi ya waislamu wanaomtuhumu kwa
kuendesha kwa siri vita dhidi ya uislamu na upendeleo wa elimu na madaraka kwa
wakristo.
Kutangazwa
mwenye Heri Kwa taratibu za Kanisa Katoliki, mchakato wa kumtangaza Mwalimu
Nyerere kuwa mtakatifu ulianza mwaka 2005, na tayari kanisa hilo kwa kibali
rasmi kutoka Roma makao ya Baba Mtakatifu, limeshamtangaza kuwa mwenyeheri.
Kuwa
mwenyeheri ni hatua ya kwanza ya kuingia utakatifu.
Wakristo wakatoliki
wameanzisha sala maalumu na kufanya maombi kwa nia ya maombezi yake ili aweze
kutangazwa kuwa mtakatifu. Ibada ya kwanza ilifanyika katika kanisa kuu la
Jimbo la Musoma, na kuongozwa na aliyekuwa askofu wa Jimbo hilo marehemu askofu
Justine Samba.
Alikuwa
mwanamichezo Licha ya Kuwa mwalimu na mwanasiasa hususani kiongozi mkuu wa nchi,
pia Nyerere alikuwa mwanamichezo, aliaznisha mchezo wa bao, akiwa Butiama
alicheza bao nyumbani kwake na majirani zake, wakati mwingine alipotembelewa na
wafuasi wake wa kisiasa alikuwa akishiriki nao kucheza bao.
Kutokana na
maisha yake aliyoyaishi ambayo yalijaa uvumilivu, unyenyekevu na uadilifu bado
anakumbukwa na watanzania hasa wa hali ya chini hasa kutokana na sera zake za
kujali utu na ubinadamu.
Ni mmoja wa
viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na kutawala
kwa miaka zaidi ya 24.
0 Comments:
Post a Comment