Ripoti ya Shirika la Watoto
la Kimataifa UNICEF nchini Madagascar linaendelea kupambana na utapiamlo na
ukosefu wa maji safi na salama.
Ripoti hiyo imesema kutoka Januari hadi Agosti
mwaka huu watoto akali ya 17,800 wenye utapiamlo walipata huduma.
Kiwango
walichojiwekea katika kusaidia watoto wa taifa hilo kwa kipindi hicho ni 17,000
hivyo kuwahudumia kiwango hicho ni kuvuka malengo.
UNICEF Madagascar imesema
watu walioko kusini mwa taifa hilo akali ya 94,894 wamepata huduma ya maji safi
na salama kupitia miundombinu ya bora ya maji.
Aidha ripoti hiyo imesema UNICEF
nchini humo iliomba kiasi cha dola milioni 8.26 kwa ajili ya watoto na familia
zao.
CHANZO:
UNICEF MADAGASCAR
0 Comments:
Post a Comment