Namibia ni taifa lililopo
kusini mwa Afrika. Upande wa Magharibi limepakana na bahari ya Atlantiki.
Pia inapakana
na mataifa ya Zambia na Angola katika mpaka wake wa Kaskazini.
Kwa upande wa
Mashariki taifa hilo linapakana na Botswana na Afrika Kusini kwa upande wa
Kusini na Mashariki.
Japokuwa taifa hilo halipakani na Zimbabwe mto Zambezi umekuwa
mpaka baina yake kwa mita zisizozidi 200.
Namibia ilipata uhuru wake kutoka Afrika Kusini Machi 21, 1990 baada ya
vita vya Uhuru vya Namibia. Mji Mkuu wa taifa hilo ni Windhoek. Namibia imekuwa
mwanachama wa Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja
wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Madola
(Commonwealth).
Ardhi ya taifa hilo no kavu yenye hali ya Jangwa. Imekuwa
ikikaliwa na watu wa jamii ya Damara na Nama. Katika karne ya 14 jamii ya
Wabantu ilihamia katika maeneo ya jamii hizo kutokana na kusambaa kwa Wabantu.
Tangu kwa wakati huo kundi kubwa la Kibantu la Aawambo limekuwa likiikalia
ardhi hiyo.
Mwaka 1878 ilikuwa chini ya Waingereza, mnamo mwaka 1884 Wajerumani
waliikalia ardhi hiyo na ikawa inaitwa German South West Africa. Wajerumani
walitengeneza miundo mbinu ya reli na kilimo.
Hata hivyo kati ya mwaka 1904
hadi 1908 kulitokea mapigano yaliyosababisha watu wengi kupoteza maisha baina
ya Waherero na Wanama.
Utawala wa Wajerumani ilifikia kikomo mwaka 1915
ukipigwa na Afrika Kusini. Hata baada ya Vita Vikuu vya Dunia kuisha taifa hilo
likasalia kuwa mikononi mwa League of Nations.
Mnamo mwaka 1966 Umoja wa Mataifa ulitangaza
kuwa utawala wake juu ya taifa hilo umeisha ndipo Afrika Kusini ilishikilia
eneo hilo kwa Sheria ya de facto.
Mnamo mwaka 1973 Umoja wa Mataifa ulikitambua
rasmi chama cha harakati za ukombozi kwenye taifa hilo cha SWAPO ambacho kwa
kiasi kikubwa kilikuwa na watu wengi wa jamii ya Aawambo.
Afrika Kusini iliweka
utawala wa mpito katika taifa hilo mwaka 1985 na ilipofika mwaka 1990 ilitoa
uhuru kamili kwa Namibia. Hata hivyo Walvis Bay na Penguin Islands ilikuwa
chini ya milki ya Afrika Kusini hadi mwaka 1994.
Namibia ina idadi ya watu
akali ya milioni 2.6 huku ikiongozwa na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi.
Kilimo,
ufugaji, utalii na uchimbaji wa madini kama Uranium, dhahabu, fedha na metali
za base zimekuwa muhimili wa uchumi wa taifa hilo ambalo kwa sasa linaongozwa
na Rais Hage Geingob ambaye alishika wadhifa huo kuanzia Machi 21, 2015.
Geingob alipokea mikoba ya Hifikepunye Pohamba.
0 Comments:
Post a Comment