Jamhuri ya Botswana ni
taifa mabalo linapatikana Kusini mwa Afrika.
Hapo awali lilikuwa likijulikana
kama koloni la Uingereza likiwa na jina la Bechuanaland.
Ilipata jina jipya
baada ya kupata uhuru wake ikiwa mikononi mwa Jumuiya ya Madola Septemba 30,
1966.
Tangu hapo imekuwa kijulikana hivyo ikiwa ni taifa ambalo chaguzi zake
zimekuwa imara bila kuyumba. Mwaka 1998 lilikuwa ni taifa ambalo lilikuwa bora
katika mapambano dhidi ya rushwa.
Ni taifa ambalo limekuwa kongwe katika
masuala ya demokrasia barani Afrika. Asilimia 70 ya taifa hilo imechukuliwa na
Jangwa la Kalahari.
Imepakana na Afrika Kusini kwa upande wa Kusini na Kusini
Mashariki, Namibia kwa upande wa Magharibi na Kaskazini na Zimbabwe kwa upande
kwa Kaskazini Mashariki.
Pia Botswana imepakana na Zambia kwa upande wa
Kaskazini karibu na eneo linalochukuliwa kuwa lina maisha ya kiwango cha chini
la Kazungula.
Taifa hilo lina takribani watu milioni mbili, likiwa katika
rekodi ya mataifa yenye idadi ya watu waliotawanyika. Ni asilimia 10 pekee ya
watu hao ndio wanaishi katika mji mkuu wake wa Gaborone.
Miaka ya nyuma
lilikuwa ni taifa maskini zaidi duniani miaka ya mwishoni mwa 1960 lakini baada
ya hapo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuweza kuwa taifa lenye uchumi unaokua
kwa kasi. Uchumi wa Botswana unategemea uchimbaji wa madini, ufugaji wa ng’ombe
na utalii.
Kwa sasa limekuwa ni taifa ambalo lina mazingira bora ya kuishi na
kuwa miongoni mwa mataifa chini ya Jangwa la Sahara yenye Maendeleo katika
kiwango cha HDI (Human Development Index).
Botswana ni mwanachama wa Umoja wa
Afrika, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Jumuiya Madola na Umoja wa
Mataifa. Hata hivyo taifa hilo lina asilimia 20 ya watu waliathiriwa na Virusi
vya Ukimwi na Ukimwi wenyewe.
Inaelezwa kuwa idadi ya watu waliokuwa na maradhi
hayo ilipanda kutoka 290,000 mwaka 2005 hadi 320,000 mwaka 2013.
Imetayarishwa na Johnson
Jabir…….Oktoba 10, 2019
0 Comments:
Post a Comment