Oktoba 25, 1944 alizaliwa
mjasiriamali na mhandisi wa taifa la China Ren Zhengfei.
Huyu ndiye mwanzilishi
na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Huawei ambali makao yake makuu yapo
Shenzhen nchini China.
Huawei ni kampuni la pili la mawasiliano kwa ukubwa
duniani kwa kuzalisha simu janja. Zhengfei ana utajiri wa dola kimarekani
bilioni 1.7 Zhengfei alizaliwa katika kaunti ya Zhenning huko Guizhou.
Babu yake alikuwa mwenyeji wa jimbo la Jiangsu na mtaalamu wa masuala ya vyakula. Baba yake alifahamika kwa jina la Ren Moxun ambaye hakumaliza masomo ya chuo kikuu. Inaelezwa sababu ya kutomaliza masomo hayo ilitokana na babu yake kufariki dunia.
Wakati wa utawala wa Japan nchini China baba yake alihamia Guangzhou na akawa mfanyakazi wa serikali ya Kuomitang katika kiwanda cha silaha akiwa kama karani. Baada ya mwaka 1949 baba yake alichaguliwa kama Rais wa kwanza wa Middle School ya Duyun ambako alikutana na mama wa Ren Zhengfei.
Mnamo mwaka 1958, baba yake alikuwa mwanachama wa Chama cha CP huku mama yake akiwa Mwalimu Mkuu wa Middle School ya Duyun.
Ren alisoma shule ya upili na baadaye chuo kikuu cha Chongqing mwaka 1960. Zhengfei alijiunga na taasisi ya jeshi la China (PLA) akifanya kazi kama fundi. Katika chuo hicho cha utafiti Zhengfei hakuwa kupata cheo chochote cha kijeshi. Muda mwingi aliutumia katika jeshi akifanikisha masuala mbalimbali ya kiteknolojia.
Mnamo mwaka 1978 alichaguliwa kwenda katika Kongamano la Kitaifa la Sayansi. Mwaka 1982 alistaafu kazi ya jeshi na kuwa raia mwaka 1983.
Zhengfei alienda zake Shenzhen na kufanya kazi zake binafsi za biashara ya kielektroniki. Mnamo mwaka 1987 Zhengfei alianzisha Huawei Technologies Co. Ltd kwa kiasi cha yuan 21,000 kwa wakati huo ilikuwa na thamani ya shilingi milioni 15 za kitanzania.
Awali Huawei ilikuwa ikiuza, ikifanya matengenezo ya switchi mbalimbali za server kwa mkataba wa uwakala na kampuni za Hong Kong nchini China.

0 Comments:
Post a Comment