Bill Gates ni mwanzilishi,
mwenyekiti na mbunifu mkuu wa programu za kampuni ya ya Microsoft, kampuni ya
programu yenye mafanikio zaidi duniani, inayoaminika kwa utengenezaji wa
programu zilizo na nguvu na ubunifu hali zikiwa bado zenye utumizi mwepesi.
Microsoft sasa inaajiri zaidi ya watu elfu hamsini na tano katika nchi
themanini na tano.
William Henry Gates III anajulikana
kama Bill Gates alizaliwa Oktoba 28, 1955 na kulelewa katika kijiji cha Seattle
pamoja na dada zake wawili. Katika umri wake mdogo Bill Gates alivutiwa na
utengenezaji wa programu akiwa katika mojawapo wa shule kijijini Seattle. Akiwa
huko shuleni Seattle, Bill Gates alikutana na Paul Allen, mwanafunzi mwenzake
wakawa marafiki. Hapo ndipo wakaanza kutumia tarakilishi ndogo ya shule
kujiendeleza ujuzi wao.
Walijiunga na kampuni ya
kompyuta, malipo yao ikiwa ni kutumia tarakilishi yenye nguvu zaidi. Kazi yao
ilikuwa ni kutafuta nukshi katika mitambo ya kompyuta, wakati huohuo waliweza
kijifunza lugha mpya za kompyuta. Bill akaenda kwenye Chuo Kikuu cha Harvard.
Kwa mara nyingine tena akajiunga pamoja na Paul kuandika toleo jipya la
programu ya Msingi wa lugha ya kwanza ya kompyuta ya kibinafsi, iitwayo Altair
8800.
Kampuni hiyo iliridhishwa na kazi ambayo Bill Gates na Paul Allen
waliofanya na programu hiyo ikapewa leseni. Jambo hili liliwachangia Gates na
Allen kuanzisha kampuni ya Microsoft, iliyokuwa ikitengenezea kampuni zingine
programu. Bill Gates aliacha masomo yake katika chuo kikuu cha Harvard na
kujishughulisha muda wake wote katika biashara.
Mapumziko yao yalikuja
walipotengeneza mfumo wa kuendesha kompyuta uitwao MS-DOS uliotumika katika
kompyuta ya kwanza ya kibinafsi ya IBM. Baadaye waliweza kuzishawishi kampuni
zingine zinazotengeneza kompyuta kutumia mfumo huo wa MS-DOS. Mfumo huu mpya wa
MS-DOS ulipata umaarufu katika soko miaka ya 1980 na baadaye, Microsoft pia
ilianza kutengeneza programu kama vile neno sindikizi.
Microsoft ilitangaza mfumo
mpya wa uendeshaji wa kompyuta uitwao Windows 1.0 mwaka wa 1983, ambao ulikuwa
na grafiksi bora na pia uliwezesha kufanya zaidi ya jambo moja kwa wakati
mmoja. Hata hivyo hakuwa bidhaa nyingine iliyotolewa miaka mbili baadaye hadi
mwaka wa 1985, kwa kuwa ni programu chache zilizoweza kuendeshwa katika mfumo
huu wa Windows 1.0. Hivyo mfumo huu mpya haukupata umaarufu vile.
Kipindi cha miaka mitano
baadaye Microsoft ilitoa mifumo mipya ya Windows 2.0 iliyokuwa bora zaidi
kuliko mifumo ya hapo awali. Kampuni ya Microsoft iliweza kupata umaarufu zaidi
katika soko la hisa, na akiwa umri wa miaka 31, Bill Gates aliweza kuwa
bilionea mchanga zaidi katika historia ya Marekani.
Katika mwaka wa 1990
Microsoft ikiongozwa na Bill Gates ilitoa toleo jipya la Windows liitwayo
Windows 3.0 na kuboreshwa kiasi GUI. Toleo hili jipya liliweza kuuzwa zaidi ya
nakala milioni kumi, likifuatiwa na matoleo mengine ya Windows 3.1, 3.11 na
makundi ya kazi ambayo yaliongeza misaada kwa mitandao. Kutokana na mafanikio
yao ya maendeleo, Microsoft ilitoa matoleo mengine ya Windows 95 ikifuatiwa na
Windows 98, 2000, Millennium Edition na toleo la sasa Windows XP.
Kila toleo
jipya lilipotolea kampuni ya Microsoft ilizidi kupata umaarufu katika soko la
hisa, ikiongezwa na baadhi ya programu kama vile Microsoft Office, michezo n.k.
Umaarufu huu umemfanya Bill Gates kuwa mtu tajiri duniani myenye thamani ya
wastani wa dola bilioni arubaini na sita.
Ubunifu wa Bill Gates wa
kutengeneza programu umekuwa mchango wake katika mapinduzi ya kompyuta na
sayansi ya kompyuta.
0 Comments:
Post a Comment