Thursday, October 31, 2019

Ushelisheli ni taifa la namna gani?




Ushelisheli ni taifa ambalo ni visiwafungu katika bahari ya Hindi likiwa kiliometa 1,500 kutoka katika Pwani ya Afrika Mashariki. 

Visiwafungu vya Comoro, Madagascar, Reunion na Mauritius vipo upande wa Kusini mwa Ushelisheli. Pia Maldives na Chagos Archipelago kwa upande wa Mashariki. Ushelisheli ina takribani watu 94,367. 

Idadi hiyo ya watu inalifanya taifa hilo la Ushelisheli kuwa ndio  lenye idadi ndogo ya watu katika bara la Afrika. Ilijiunga na Umoja wa Afrika baada ya kupata uhuru wake mwaka 1976. 

Kutoka wakati huo hadi sasa Ushelisheli limekuwa ni taifa linalokuwa kiuchumi likiegemea zaidi katika kilimo na utalii. Mapema mwanzoni mwa mwaka 2010 Rais wa Taifa hilio Danny Faure alipeleka mipango yake katika Bunge la nchi hiyo kwa ajili ya kuhamasisha uwekezaji nchini humo. 

Hali hiyo imelisaidia taifa hilo kuwa na uchumi bora kwani hadi sasa ndilo taifa pekee katika bara la Afrika lenye uchumi wa juu kuliko jingine. Hata hivyo kuwa na kiwango bora cha juu katika masuala ya uchumi hakujafanikiwa sana kuondoa umaskini. 

Mfumo wa sias ala taifa hilo ni kwamba Rais ndiye kiongozi wa nchi na mtendaji mkuu serikali. Anachaguliwa kwa kupigiwa kura na kukaa madarakani wa miaka mitano. 

Bunge la Ushelisheli lina wajumbe 34 huku 25 wanachaguliwa kwa kupigiwa kura kila miaka mitano. 

Mfumo wa sheria wa taifa hilo ulianzishwa mwaka 1903 ukianzisha katika mahakama ya mwanzo hadi mahakama ya rufani. Chama kilichotawala taifa hilo ni kile cha PP hadi mwaka 2009 kilipobadilishwa jina na SPPF. 

Hata hivyo mnamo Novemba 2018 chama hicho kimebadili jina lake na kuwa Muungano wa Ushelisheli (US). Dini ya Kikristo nchini humo ndiyo yenye wafuasi wengi ikichukua asilimia 76.2 ikifuatiwa na Uhindu unaochukua asilimia 2.4 huku Uislamu ukishika nafasi ya tatu kwa asilimia 1.6 ya idadi ya watu katika Ushelisheli. 

Katika michezo mpira wa kikapu ndio unaongozwa kwa kupendwa nchini humo. Tangu mwaka 2015 taifa hilo limekuwa likipambana na mataifa makubwa kama Misri katika mchezo huo. Mji mkuu ni Ushelisheli ni Victoria.


Imetayarishwa na Jabir Johnson………………………………Oktoba 31, 2019
 

0 Comments:

Post a Comment