Mwanamke mwenye umri wa
miaka 36 amefikishwa katika vyombo vya sheria nchini Namibia kwa kujaribu
kumuua mwanaye wa miaka mitatu kwa kumchoma na kisu huku mtoto wake wa miezi
miwili na miaka sita wakinusurika.
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya
Keetmanshoop imesema kuwa tukio hilo alilitenda siku ya Jumamosi huku dhamira
yake ikiwa bado haijafahamika.
Mahakama hiyo imemtaja
mwanamke huyo kuwa ni Elfriede Stoffel, mama wa watoto watatu hakutakiwa kujibu
lolote na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 6 mwaka huu itakapotajwa tena.
Mwendesha mashtaka wa
serikali Coleen Yisa ameita mahakama kutompa dhamana mwanamke huyo kutokana na
aina ya kosa alilolitenda.
Mwendesha mashtaka huyo
ameiambia mahakama hiyo kuwa endapo angepewa dhamana ingeondoa umuhimu wake kwa
jamii kwani alichokifanya ana kesi ya kujibu kwa manufaa ya jamii.
Mwanamke huo ameonyesha nia
yake ya kupata msaada wa kisheria.
Kwa upande wake David
Indongo Kamishna Msaidizi wa Polisi wa Kharas aliviambia vyombo vya habari juzi
Jumapili kuwa mhanga amelazwa katika hospitali ya Keetmanshoop.
Indongo aliongeza kuwa
mwanamke huyo alimchoma kwa kitu chenye ncha kali na kuacha alama katika
mgongo.
Aidha mhanga huyo ambaye ni
mtoto wa kike anaendelea vizuri baada ya kupata huduma.
Kamanda Indogo aliongeza
kuwa baada ya kutekeleza unyama huo, alitokwa na machozi na kuonyesha kujutia
kitendo alichomfanyia bintiye yake.
Mashuhuda wa tukio hilo
ambao ni ndugu zake walisema kuwa ndugu yao ana matatizo mengi sana ambayo
yanamfanya awe na msongo wa mawazo.
Siku ya tukio walisema
mwanamke huyo alijifungia na watoto wake watatu wa miezi miwili na mwingine wa
miaka sita na aliyetendewa ukatili huo.
Kelele za watoto waliokuwa
wakipiga ziliwashtua mashuhuda hao na kukimbia kwenda kutoa msaada na walipofungua
mlango walikuta tayari ameshamchoma bintiye.
Vyanzo vingine vinadai kuwa
wasingewahi alikuwa na madhumuni ya kuwamaliza wanaye wote watatu. Hata hivyo
katika siku za karibu nchini humo kumekuwa na matukio ya kustaajabisha likiwamo
la babu mwenye umri wa miaka 69 kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka 14.
Mahakama ya Keetmanshoop
imesema mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Aron Basson alifikishwa
kizimbani kwa kosa la kubaka na kutishia.
Pia mkazi wa Rehoboth huko Kuvukiland
mwenye umri wa miaka 22 aliyefahamika kwa jina la Ruben Losper alikwenda kwa
girlfriend wake wa zamani na kumchoma visu mara tano katika kifua kasha naye
kujiua.
Msichana aliyefahamika kwa
jina la Bianca va Wyk (22) alifariki dunia akiwa kwenye harakati za kufikishwa
hospitali.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Naibu
Kamishna Edwin Kanguatjivi amesema kijana huyo alijiua kwa kujinyonga kwa waya
kwenye mti usiku wa kuamkia jana huku chanzo kikiwa bado hakijafahamika.
0 Comments:
Post a Comment