Imeelezwa kuwa watu 2,000
wamefariki dunia kutokana na maradhi ya ebola kwa zaidi ya mwaka mmoja
mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Maradhi hayo yanayoendelea
kulitesa taifa hilo yamekuwa ni mabaya zaidi ikilingwanishwa na yale ya Afrika Magharibi
ya mwaka 2014-2016.
Licha ya kuwapo kwa kila juhudi za kupambana na maradhi
hayo lakini idadi ya watu wanapewa chanjo ya kuzuia maradhi hayo imekuwa ndogo. Shirika la kujitolea la MSF linasema mwendo
umekuwa wa kusuasua kwa watu wa taifa hilo kupata chanjo dhidi ya Ebola.
Hata hivyo
MSF imetoa mapendekezo yake kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) kupunguza mipaka
ya utoaji wa chanjo ili kwenda kwa kasi zaidi na kulitaka shirika hilo liunde
kamati ya kusimamia programu za chanjo ya Ebola.
Mratibu wa huduma za dharura wa MSF Dkt.
Natalie Roberts anasema kinachofanywa na WHO ni sawa na kuwapa ndoo ya maji kwa
ajili ya kuzima moto kisha kuwataka kutumia kimoja kwa ajili ya kuzima moto.
Aidha
Dkt. Natalie ameipongeza wizara ya Afya na WHO licha ya kuweka mpaka wa chanjo
takribani watu 220,000 wamepata chanjo ya Ebola ya rVSV-ZEBOV na utafiti wa chanjo
uliofanywa na Merck umeonyesha uwezo mkubwa wa kufanya kazi.
Mratibu wa Kampeni
za MSF Dkt. Isabelle Defourny anasema wapo mbioni kuongeza kasi ya utoaji wa
chanjo pale inapobidi; kwani matarajio ni watu 2,000-2,500 kwa siku ikilinganishwa na idadi ya sasa ya watu
500-1,000.
0 Comments:
Post a Comment