Septemba 21, 1954 alizaliwa
mwanasiasa na Waziri Mkuu wa sasa wa Japan Shinzo Abe.
Leo anatimiza miaka 65
tangu alipoliona jua. Alizaliwa jijini Tokyo. Abe ametoka katika familia ya
kisiasa na kijeshi kwani mababu zake waliwahi kuwa wanasiasa na wanajeshi wakati
wa vita vya pili vya Dunia (WWII). Kwa asili familia yake imetokea Yamaguchi
mojawapo ya mji ambao una historia kubwa nchini Japan. Mara ya kwanza Abe
kuonekana katka siasa za Japan ilikuwa ni mwaka 1993 alipochaguliwa kuwa
mwakilishi katika Baraza la Wawakilishi kutoka Yamaguchi. Hatua hiyo ilikuja
baada ya kifo cha baba yake mwaka 1991. Abe alishinda kwa kura nyingi. Pia Abe
amewahi kushika nyadhifa za ndani ya
serikali ya Japan kati ya mwaka 2000 na 2003. Aliwahi pia kushika
wadhifa wa Katibu Mkuu wa Chama cha Liberal Democratic (LDP). Akiwa na umri wa
miaka 52 hiyo alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Japan. Hiyo ilikuwa Julai 14,
2006 alipoweka rekodi ya kwanza taifa hilo kuwa na Waziri Mkuu mwenye umri mdogo
baada ya Fumimaro Konoe aliyeshika wadhifa huo mwaka 1941. Wadhifa huo aliushika
kwa mwaka mmoja hadi 2007. Mnamo Desemba 26, 2012 Abe alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu
wa Japan kwa kura 328 kati ya 480 ya wabunge.
0 Comments:
Post a Comment