Tuesday, September 17, 2019

MAKTABA YA JAIZMELA: Narendra Modi ni nani?

Septemba 17, 1950 alizaliwa mwanasiasa na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi. 

Waziri Mkuu huyo pia ni kiongozi wa chama cha Bharatiya Janata (BJP). Mwaka 2014 alikiongoza chama hicho kwenye uchaguzi wa Bunge dogo la India ‘Lok Sabha’ ambako waliibuka na ushindi, baada ya kuapishwa kuwa Waziri Mkuu wa taifa hilo. Kabla ya kuwa Waziri Mkuu wa India Modi alikuwa chief minister wa Jimbo la Gujarat lililopo Magharibi mwa India. Modi alizaliwa katika mji mdogo wa Vadnagar nchini India. Alikulia katika jimbo la Gujarat. Akiwa huko alihitimu masomo ya uzamili katika masuala ya Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Gujarat mjini Ahmadabad. Alijiunga na jumuiya ya Kihindu ya Rashtriya Swayamsevak Sangh (RSS) mwanzoni mwa miaka ya 1970. Mnamo mwaka 1987 alijiunga na BJP na mwaka uliofuata alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho mjini Gujarat. Mwaka 1990 Modi alikuwa miongoni mwa wajumbe walioshiriki katika serikali ya muungano katika jimbo hilo na alikisaidia chama hicho kwa mafanikio mwaka 1995. Modi alizama katika kinyang’anyiro cha kwanza Februari 2002 kuwania nafasi ya ubunge wa jimboo hilo la Gujarat na alifanikiwa.

0 Comments:

Post a Comment