Thursday, September 26, 2019

Burundi ni taifa la namna gani?


Burundi ni miongoni mwa mataifa madogo kabisa barani Afrika huku likiwa na idadi ya takribani watu milioni 10.5 

Idadi hiyo ya watu inaifanya Burundi kukalia nafasi ya 86 ya kuwa na idadi kubwa ya watu. Burundi ni taifa lililoko katika Ukanda wa Maziwa Makuu likiwa limepakana na Rwanda kwa upande wa kaskazini, Tanzania kwa upande wa Mashariki na Kusini Mashariki na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa upande wa Magharibi. 

Ziwa Tanganyika kwa upande wa Kusini Magharibi. Mji Mkuu ni Gitega kwa sasa ambao umeanza kutumika Februari 2019 wakihama Bujumbura. Wa-Twa, Wahutu na Watutsi ndio makabila ambayo yanaelezwa kuishi katika ardhi hiyo kwa takribani mika 5,000 iliyopita. 

Kwa zaidi ya karne mbili Burundi ilikuwa ni dola huru hadi mwanzoni mwa karne ya 20 pale wakoloni wa Kijerumani walipoanza kutawala eneo hilo. Baada ya kuanguka kwa utawala wa Adolf Hitler, Burundi ilikaliwa na Wabelgiji. Mnamo mwaka 1962 ilijipatia uhuru wake lakini hadi mwaka 1966 ndipo ilipoanza kutumia mfumo wa chama kimoja. 

Hata hivyo matukio ya mauaji na vitendo vya kikatili vilisababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwaka 1970 na 1990 hali ambayo imefanya kuwa taifa maskini ulimwenguni. Mauaji ya kimari ya Wahutu ya mwaka 1994 yalileta taswira tofauti nchini humo. 

Mnamo mwaka 2015 Rais wa sasa Pierre Nkurunziza aliendelea katika kipindi cha tatu cha kushikilia wadhifa huo hatua mabayo ilipingwa na jumuiya za kimataifa. 

Machi 13, 1992 Rais wa Watutsi Pierre Buyoya aliandika katiba ambayo iliwafanya Warundi waingie katika mfumo wa vyama vingi ambapo hadi sasa vyama vya siasa 13 vimesajiliwa nchini humo. 

Mnamo Juni 6, 1998 katiba hiyo ilibadilika na kupanua bunge la nchi hiyo na kuongeza nafasi ya kuwa na makamu wawili wa rais katika taifa hilo. 

Mkataba wa Arusha uliifanya Burundi kuunda serikali ya mpito mnamo mwaka 2000. Oktoba 2016 Burundi ilionyesha nia yake ya kutaka kujitoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu  (ICC). 

Hata hivyo Burundi inasalia kuwa taifa ambalo lina jamii kubwa ya vijijini kuliko mjini mnamo mwaka 2013 asilimia 13 ya watu ndio wanaoishi mijini. 

Idadi kubwa ya wahutu (85%), Watutsi (15%) na chini ya asilimia moja ni Wa-Twa wanajihusisha na kilimo na ufugaji.
Rais Pierre Nkurunziza

Imetayarishwa na Johnson Jabir…..Septemba 26, 2019

0 Comments:

Post a Comment