Monday, September 30, 2019

Ufahamu mwezi Septemba

Septemba ni mwezi wa tisa wa mwaka katika kalenda ya Julian na kalenda ya Gregori. Septemba ni mwezi wa tatu kati miezi minne ambayo ina siku 30. 

Pia ni mwezi wan ne kati ya mitano ya mwaka yenye siku chini ya 31. September ni neno ambalo limechukuliwa kutoka katika lugha ya Kilatini ‘Septem’ ikiwa na maana ya ‘Saba’. Sasa ilikuwaji mpaka ikawa ni tisa katika mtiririko wa miezi? 

Hii ilitokana na Kalenda ya zamani ya Kirumi ambayo ilikuwa na miezi 10, ile kalenda ya Romulus mwaka 750 K.K ambayo mwezi wa kwanza ulikuwa ni Machi (kilatini ikifahamika kama Martius. 

Wanahistoria wanasema kalenda hiyo ilidumu hadi mwishoni mwa mwa 451 K.K Kuanzi hapo kulifanyika mabadiliko makubwa ya kalenda ambapo iliongezwa miezi miwili Januari na Februari ambayo waliiweka mwanzoni, hivyo Septemba ukaanza kuonekana kuwa ni mwezi wa tisa katika mtiririko huo. 

Hakukuwa na haja ya waliokuwepo kubadili jina la 'Septem' kutoka katika maana ya asili  wakaamua kuliacha kama lilivyo hadi leo. Pia kabla ya kubadilishwa mwezi Septemba ulikuwa na siku 29 hadi wakati ambapo kalenda ya Julian ilipofanya maboresho hayo na kuongeza siku moja na kuwa na 30 kama ambavyo unafanya sasa.  

Aidha Septemba umekuwa ni mwezi ambayo kila jamii imekuwa ikiuchukulia kulingana na mila na desturi zao. Kwa mfano makanisa ya Eastern Orthdox yamekuwa yakiuchukuliwa kuwa ni mwezi wa kikanisa ambapo hutakiwa kuingia katika mfungo na kuhitimishwa kwa sherehe. 

Nchi nyingi za upande wa kaskazini mwa dunia nikimaanisha Ulaya na maeneo mengine ya upande huo huuchukulia mwezi Septemba kama mwanzo wa mwaka wa masomo ambapo wanafunzi huwa wanarudi mashuleni na vyuoni baada ya mapumziko.   

Kama haitoshi mwezi Septemba huchukuliwa kuwa ni mwezi wa mavuno katika Kalenda ya Charlemagne. Hii ni kutokana na kumbukumbu ya utawala wa Mfalme wa Warumi maarufu Charles, The Great I aliyezaliwa Aprili 2, 742 na kufariki dunia Januari 28, 814.

Charlemagne aliitawala Dola la Rumi kuanzia mwaka 800 hadi 814. Katika kujiimarisha kiuchumi na kisiasa Charlemagne aliamua kuwa na kalenda hiyo. Huo ni kwa ufupi kuhusu mwezi Septemba.



CHANZO: KILIFM HABARI

0 Comments:

Post a Comment